Skip to main content
  • Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama, Aipongeza MSD kwa Manunuzi Vifaa Tiba vya Mama na Mtoto

    Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama ameipongeza Bohari ya Dawa (MSD) kwa kuendelea kuhakikisha inanunua vifaa muhimu vinavyohitajika kusaidia kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa wakiwa Njiti.

    Waziri Mhagama amesema hayo leo wakati akikabidhi vifaa tiba maalumu vya kuwasaidia watoto wenye matatizo kupumua, ambavyo amevikabidhi kwa  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Dkt. Mohammed Mang'una kwa niaba ya Waganga Wakuu wote nchini. 

  • Kamati ya Bunge ya Afya na UKIMWI, Yaridhishwa na Utekelezaji wa Mradi wa Gloves - MSD Idofi

    Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, yaeleza kuridhishwa na hatua za utekelezaji wa mradi wa Kiwanda cha kuzalisha Mipira ya Mikono cha MSD, kilichoko idofi, Makambako Mkoani Njombe.

    Hayo yameelezwa agosti 7, 2024 na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe.Christina Mnzava, wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi huo kwa lengo la kukagua na kupokea taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo.

    Mhe. Mnzava kwaniaba ya kamati hiyo, amepongeza juhudi mbalimbali zilizochukuliwa na MSD, katika kuendeleza mradi huo, ambayo umetoa ajira kwa wananchi wa eneo hilo.

  • Viongozi wa Sekta ya Afya Wahimizwa Kushirikiana na MSD

    MOROGORO.

    Wasimamizi na wadau wa afya mkoani Morogoro, wameaswa kushirikiana kwa ukaribu na Bohari ya Dawa (MSD), ili kwa pamoja waweze kutatua na kuboresha hali ya upatikanaji wa bidhaa za afya mkoani humo, kwa ajili ya ustawi watu na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

    Rai hiyo imetolewa hii leo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wà Morogoro, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mjini Mhe. Rebeka Nsemwa, wakati akifungua kikao kazi cha wateja na wadau wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, kilichokutanisha viongozi wa sekta ya afya ngazi ya mkoa na wilaya mkoani humo.

  • SADC Yazindua Kanzidata ya Mfumo wa Taarifa za Bidhaa za Afya Kwa Nchi Wanachama

    Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imezindua kanzidata maalum kwa ajili ya ukusanyaji na usindikaji wa taarifa za dawa na vifaa tiba kutoka kwa wazalishaji na wauzaji mbalimbali duniani, ambapo mfumo huo utarahisisha upatikanaji na ununuzi wa bidhaa za afya kutoka nchi wanachama.

    Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 14/05/2024 jijini Dar es Salaam, na kushuhudiwa na Bohari za Dawa za nchi za SADC, pamoja na viongozi mbalimbali wa Sekta ya Afya wa jumuiya hiyo, waliokutana kwa siku mbili jijini humo.

  • Wataalamu wa Afya Kutoka Sierra Leone, Wafanya Ziara ya Mafunzo MSD

    Wataalamu wa Afya kutoka nchini Sierra Leone leo wametembelea Bohari ya Dawa (MSD) kwa lengo kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu shughuli za Ugavi, Uhifadhi, Uendeshaji, Ununuzi, Huduma kwa Wateja, Sera, Udhibiti Ubora, pamoja na mambo mengine yanayohusu mnyororo wa Ugavi wa bidhaa za afya.

    Akiongea kwa niaba ya Wizara ya Afya wakati wa kuukaribisha ujumbe huo nchini, Mfamasia Mkuu wa Serikali Daudi Msasi, amesema ujio wa wageni hao ni ishara kwamba kama nchi tumeboresha na kuimarisha Bohari yetu katika utoaji wa huduma, ndio maana wengine wanakuja kujifunza.

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.