Kitengo cha Usafirishaji
Kitengo cha Usafirishaji, ni kitengo chini ya Kurugenzi ya Ugavi na Uendeshaji, ambacho husimamia vyombo vya usafiri vya MSD na kuratibu usambazaji wa bidhaa za afya kwenda kanda zote kumi na vituo teule nchini Tanzania.
Kitengo hiki kina magari zaidi ya 215, yakiwamo malori ya mnyororo baridi wa bidhaa za afya. Kitengo hiki huhakikisha bidhaa za afya zinasafirishwa na kufikishwa salama, kwa wakati, na kwa ukamilifu. Kitengo huratibu mipango ya usafirishaji ya kila wiki inayowasilishwa na Kanda zote za MSD, hupanga magari, husimamia shughuli za upakiaji, na kufuatilia bidhaa zilizopakiwa kwa kutumia mfumo wa kisasa wa usimamizi wa magari.
Ili kuhakikisha ufanisi na ubora wa bidhaa za afya, magari haya hukaguliwa na kufanyiwa ukarabati muhimu mara kwa mara katika karakana ya MSD, na kuhakikisha mifumo ya udhibiti joto inakidhi ubora wa bidhaa za afya wakati wa safari. Pia, Kitengo husaidia taasisi nyingine za serikali kwa kuzipatia huduma ya usafiri pale inapobidi.
Kitengo cha Usafirishaji ni kiungo muhimu cha mnyororo wa ugavi wa MSD, na huakikisha shughuli za usambazaji wa bidhaa za afya zinatolewa kote nchini bila kukoma. Uaminifu, usalama, na ubora wa huduma unathibitisha dhamira ya MSD ya kuhakikisha bidhaa za afya zinapatikana wakati wote nchini.