Kanda ya Dodoma
Kanda ya MSD Dodoma ilianzishwa mwaka 2007 na inatumika kama kitovu kikuu cha usambazaji wa bidhaa za afya katika eneo la kanda ya kati nchini Tanzania. Kanda hii inahudumia mikoa ya Dodoma, Singida, na Wilaya ya Kiteto (Mkoa wa Manyara) kutokana na ukaribu wa kijiografia na urahisi wa usafirishaji bidhaa. Kanda ya Dodoma inatekeleza jukumu muhimu la kuhakikisha kuna upatikanaji wa bidhaa za afya za uhakika na kwa wakati.
Mawanda ya Huduma
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi nchini Tanzania ya mwaka 2022, Kanda ya Dodoma inahudumia jumla ya watu 5,445,988, ikihakikisha kuna upatikanaji dawa na vifaa tiba wa uhakika. Kwa mujibu wa sensa,
Mkoa wa Dodoma - watu 3,085,625,
Mkoa wa Singida - watu 2,008,058
Wilaya ya Kiteto (Mkoa wa Manyara) – watu 352,305
Kwa upande mwingine, Kanda ya Dodoma inahudumia jumla ya vituo 827 vya kutolea huduma za afya, ikijumuisha vituo kuanzia ngazi ya msingi, ngazi ya kati, hadi ngazi ya taifa.
1. Vituo ngazi ya kati na taifa – Hospitali 1 ya Rufaa ya Kanda, hospitali bobezi 1 na hospitali 2 za Rufaa za Mikoa.
2. Vituo ngazi ya msingi – Hospitali 20 za wilaya zilizo chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – (TAMISEMI), vituo vya afya 116, zahanati 652, hospitali za kidi kumi na mbili (12), na hospitali nyingine ishirini na tatu 23 (hospitali za kijeshi, binafsi, na vituo vya elimu).
3. Vituo vya Tasisi za kidini na taasisi nyingine za umma - Taasisi za dini 12, na taasisi nyingine 23.
Uwezo wa Kuhifadhi na Utendaji
Ili kuhudumia vituo vya afya ipasavyo na kwa ufanisi, kanda hii ina ghala lenye ukubwa wa eneo la mita za mraba 6,534 na magari 14 ya usambazaji yenye ukubwa tofauti kulingana na mahitaji. Rasilimali hizi kwa pamoja huiwezesha Kanda kutunza, kuhifadhi, na kusambaza dawa na vifaa tiba kwa ufanisi kwa kuzingatia viwango vya juu vya ubora na usalama.
Mafanikio ya kanda ya Dodoma yanatokana na uwapo wa timu ya wataalamu 38 ikihusisha wabobezi wa masuala ya ugavi ,wafamasia, wahasibu, wawakilishi wa mauzo, maofisa huduma kwa wateja, mafundi sanifu vifaa tiba na madereva. Mchango wao wa kitaalamu unahakikisha kuwa kanda hii inaendelea kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, hivyo kuboresha utoaji wa huduma za afya na kuongeza ufanisi wa usambazaji katika maeneo yake.
Utoaji wa Huduma Bora
Kwa kuzingatia eneo lake la kimkakati, miundombinu ya kisasa, na nguvu kazi yenye ujuzi, Kanda ya MSD Dodoma inaendelea kuwa mhimili muhimu katika kuboresha utoaji wa huduma za afya katika mikoa ya Kandaa ya kati nchini Tanzania.
Kanda hii inaendelea kujidhatiti kutekeleza dira kuu ya MSD ya kuwa "Kituo Bora cha Umahiri katika Mnyororo wa Ugavi wa Vifaa Tiba Barani Afrika."