Ruka kwenda maudhui makuu

Uhifadhi

Bohari ya Dawa (MSD) ina mtandao madhubuti wa maghala yaliyowekwa kimkakati katika maeneo mbalimbali nchini, ili kuhakikisha kunakuwa na uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya wenye ufanisi. Maghala yote ya MSD yamewekwa vifaa maalum vinavyohifadhi bidhaa zenye asili ya ubaridi, (cold chain) na joto la kawaida kutegemea na uhitaji wa bidhaa husika. Kwa kutumia  mifumo ya kisasa ya uhifadhi na usimamizi wa bidhaa, sambamba na taratibu madhubuti za mnyororo wa ugavi.

MSD inahakikisha upatikanaji wa bidhaa za afya zenye viwango stahiki kupitia mtandao wake wa maghala ulioko nchi nzima, na hivyo kuboresha utoaji wa huduma za afya za uhakika. MSD imeajiri wataalam wabobezi wa bidhaa za afya na mnyororo wa ugavi ambao uhakikisha usalama wa bidhaa nyakati zote. 

Katika jitihada za kuboresha huduma, MSD inaendelea kuongeza miundombinu yake ya uhifadhi wa bidhaa za afya kwa lengo la kuongeza tija na ufanisi katika upatikanaji wa bidhaa za afya. Mnamo mwaka 2024/25, Bohari ya Dawa ilikamilisha ujenzi wa maghala mawili ya kisasa yaliyopo mikoa ya Mtwara na Dodoma, yenye ukubwa wa mita za mraba 4,800 na 7,200 mtawalia. 

Pamoja na hivyo, Bohari ya Dawa inajenga maghala mengine mikoa ya Geita, Dar es Salaam na Mwanza ikiwa ni awamu ya pili ya uboreshaji wa miundombinu. Awamu ya tatu ya ujenzi wa maghala itafanyika mikoa ya Ruvuma na Arusha lengo likiwa ni kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi na kuongeza uhifadhi kutoka mita za mraba 55,405.47 za kuhifadhia bidhaa za afya.

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.