Kitengo cha Huduma za Sheria
Kitengo cha Sheria kinahakikisha kuwa Bohari ya Dawa (MSD) inatekeza majukumu yake, kwa kuzingatia mifumo ya kisheria, vigezo na miongozo inavyoongoza taasisi za umma nchini Tanzania. Kama mshauri wa sheria wa MSD, kitengo hiki hulinda uadilifu wa taasisi, hutoa ushauri wa kitaalamu, na kusimamia uzingatiaji sheria ili kulinda sifa ya MSD na maslahi yake.
Kitengo hiki kinafanya kazi kama kiunganishi rasmi kati ya MSD na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hutoa huduma za ushauri kwa Bodi ya Wadhamini, Menejimenti, kurugenzi na vitengo vyote. Kitengo cha sheria hupitia mikataba, kanuni za ndani na makubaliano ili kuhakikisha kuwa yanawiana na sheria husika, kulinda msimamo wa MSD na kupunguza vihatarishi vinavyoweza kutokea.
Kitengo cha Sheria husimamia uzingatiaji wa sheria za taasisi na kusimamia usuluhishi wa kesi zinazohusisha taasisi, huratibu mikutano ya Bodi ya Wadhamini na vile vya Menejimenti kwa kutoa usaidizi wa kiofisi na kuhakikisha uzingatiaji wa taratibu za kisheria na utawala.
Kwa kupitia mbinu thabiti za kiutendaji, Kitengo cha Sheria huhakikisha uwazi, uwajibikaji, na utawala bora katika ofisi za MSD, kwa kuhakikisha kila uamuzi unaofanyika na ubia unaoingiwa na taasisi ni halali kisheria, na unachangia uaminifu na uthabiti wa jumla wa mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya nchini Tanzania.