Ruka kwenda maudhui makuu

Kitengo cha Kuzingatia Mkataba


Kitengo cha Mikataba ni mojawapo ya vitengo vilivyo chini ya Kurugenzi ya Ugavi na Uendeshaji. Kitengo hiki kilianzishwa mwezi Februari 2023 kwa lengo kuu la kuboresha ufanisi wa ununuzi wa MSD kwa kuingia mikataba sahihi, inayosainiwa na pande zote mbili (MSD na Mshitiri) na inafungwa na sheria ili kutimiza vigezo, masharti na matakwa yaliyowekwa kisheria. 


Kitengo kinahakikisha kuwa matakwa yote ya kimkataba kati ya taasisi na wasambazaji yanatekelezwa ipasavyo, kulingana na makubaliano yaliyofikiwa. Mchakato huu unajumuisha kupitia mikataba ili kuhakikisha inazingatia matakwa ya kisheria na kibiashara, kufuatilia utekelezaji wa mikataba, kuhakikisha bidhaa na huduma zinawasilishwa kwa wakati, kutathmini utekelezaji wa mikataba na utendaji kazi.


Kitengo hiki hufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mikataba, huku majukumu yake mengine ikiwa ni pamoja na; Kushirikiana na Kurugenzi ya Ununuzi (PMU) kusimamia utekelezaji wa mikataba yote iliyosainiwa, Kuhakikisha mikataba inatekelezwa kwa kuzingatia sheria husika, Kufuatilia uwasilishaji wa bidhaa za afya kulingana na muda uliopangwa kwenye  mkataba, Kuwasiliana na Kurugenzi ya Ununuzi (PMU) endapo kutahitajika mabadiliko au marekebisho yoyote ya mkataba, Kuwasiliana na washitiri kuhusu masuala yanayohusu utekelezaji wa mkataba, Kujibu barua na kushughulikia malalamiko yote ya washitiri yanayohusiana na utekelezaji wa mikataba, Kutathmini utekelezaji wa huduma au uwasilishaji bidhaa za afya kutoka kwa washitiri ili kubaini washitiri wasiokidhi masharti na kupendekeza hatua stahiki za kuchukuliwa, Kuhifadhi kumbukumbu zote za usimamizi wa mikataba.


Umuhimu wa kuwepo kitengo hiki ni;
Kufuatilia kwa karibu na kusimamia mikataba yote ya ununuzi wa bidhaa za afya inayoingiwa kati ya MSD na washitiri.
Kuimarisha mawasiliano kati ya MSD na washitiri.
Kushughulikia changamoto zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa mikataba.
Kufuatilia kwa karibu washitiri ili kuhakikisha uwasilishaji wa bidhaa za afya kwa wakati na kuongeza upatikanaji wa bidhaa hizo gtkupitia mikataba iliyotolewa.
Kufuatilia ukusanyaji wa bidhaa za afya zilizokataliwa kutokana na kutokidhi viwango vilivyokubaliwa, ili kuhakikisha washitiri wanawajibika kulingana na sheria na masharti ya mikataba.
Kubaini washitiri wasiotekeleza mikataba kwa mujibu wa makubaliano.

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.