Ruka kwenda maudhui makuu

Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma


Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Uhusiano (CPRU) ni kitovu cha kimkakati cha mawasiliano cha MSD, chenye jukumu la kutoa ushauri kuhusu mawasiliano ya nje na ndani, vyombo vya habari, ushirikishwaji wa wadau na  uhusiano kwa umma. 


Kitengo cha CPR kinasimamia chapa na taswira ya MSD kwa kuimarisha hadhi na mwonekano wa taasisi, kukuza uhusiano na wadau, wabia na jamii kwa ujumla. Kitengo hiki ni daraja la mawasiliano kati ya MSD na wadau wake, kikilenga kujenga uhusiano mwema, kukuza imani, na kudumisha sifa kama taasisi inayoongoza katika usimamizi wa mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya.


Majukumu makuu ya kitengo hiki ni pamoja na kuandaa na kutekeleza mikakati ya mawasiliano, kusimamia mawasiliano ya ndani na nje ya taasisi, kushughulikia masuala yanayohusiana na vyombo vya habari na kuhakikisha uthabiti wa chapa na ujumbe katika majukwaa yote ya mawasiliano. 


Kwa kuoanisha shughuli za mawasiliano na malengo ya kimkakati ya MSD, kitengo cha CPR kina jukumu muhimu katika kuendeleza dhamira ya taasisi na kuimarisha imani ya wadau wake.
 

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.