Ruka kwenda maudhui makuu

Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani

Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, kilianzishwa na Bodi ya Wadhamini ya MSD, na kinafanya kazi chini ya usimamizi wa Bodi ya Wadhamini, Bodi ya Ukaguzi na Kamati ya Vihatarishi, kikiongozwa na Mkataba wa Ukaguzi wa Ndani na Mkataba wa Kamati ya Ukaguzi na Vihatarishi. Kitengo kinafanya kazi kwa kujitegemea ili kutoa huduma za uhakika  na ushauri ambazo zitaimarisha utawala wa MSD, udhibiti wa vihatarishi na mifumo ya udhibiti.


Kitengo kikiongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani, ambaye kiutendaji anaripoti kwa Bodi ya wadhamini ya MSD na kiutawala kwa Mkurugenzi Mkuu, kinahamasisha uwazi, uwajibikaji, na uboreshaji endelevu wa shughuli zote za MSD. Kitengo kina timu ya wataalamu wa fani mbalimbali ikijumuisha wataalamu wa uhasibu, fedha, ununuzi na TEHAMA, ili kuhakikisha shughuli za kitengo zinafanyika kwa ufanisi na weledi.


Kitengo kinahakikisha mwongozo wa Kimataifa wa Uzingatiaji Utaalamu (IPPF) unasimamiwa ipasavyo, na kufanya tathmini kuhusu kuzingatia sheria na kudhihirika kwa ujumla kinazingatia viwango vya ubora vya kimataifa.


Kwa kupitia weledi, umahili na matumizi ya takwimu katika kuchagiza dhamira ya utendaji bora, Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani  huimarisha uwezo wa MSD wa kutoa huduma bora za afya na kuimarisha sifa ya taasisi ya kuhakikisha inaongoza katika mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya nchini na barani Afrika.
 

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.