Kitengo cha Mipango ya Mahitaji na Ugavi
Kitengo cha Mipango ya Mahitaji na Ugavi (DSPU) kina jukumu la kuratibu shughuli za upangaji wa ugavi wa MSD, kuhakikisha usimamizi bora wa bidhaa na usambazaji wa bidhaa za afya kwa ufanisi katika nchi nzima. Kikiwa kama msimamizi wa mzunguko wa bidhaa wa MSD. kitengo hiki hufuatilia, kukadiria na kuongeza bidhaa ili kudumisha uwiano kati ya mahitaji na ugavi.
Kitengo hushirikiana kwa karibu na Wizara ya Afya, kanda za MSD na wadau wengine, DSPU huhuisha mara kwa mara mipango ya ununuzi na viwango vya bidhaa kulingana na makadirio ya kitaifa na mahitaji ya ziada ya vituo vya afya. Kitengo hiki hufanya mapitio na ufuatiliaji wa mara kwa mara ili kupunguza hatari za ongezeko kubwa au upungufu wa bidhaa ili kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa ufanisi na kupunguza uwezekano wa upotevu wa bidhaa.
DSPU pia huongoza vikao vya Mipango ya Uendeshaji na Ugavi (O&SP) vinavyokutanisha timu za mnyororo wa ugavi kujadili upatikanaji wa bidhaa, usimamizi wa bidhaa zinazosafirishwa na uongezaji wa bidhaa. Kupitia ushirikiano na Kitengo cha TEHAMA, timu hutumia uchambuzi wa takwimu na mfumo wa ERP kuboresha usahihi wa matarajio, kutoa uamuzi, na kutekeleza mikakati mipya ya kidijiti kama mbinu ya kutumia data kwa ufanisi.
Kwa kudumisha mbinu ya uchambuzi wa takwimu na utendaji, Kitengo cha Mipango ya Mahitaji na Ugavi kinaunga mkono dhamira ya kimkakati ya MSD ya kusambaza bidhaa muhimu za afya kwa ufanisi, kuaminika na kwa njia endelevu kote Tanzania.