Ruka kwenda maudhui makuu

Kitengo cha Huduma kwa Wateja


Kitengo cha Huduma kwa Wateja ni chombo muhimu katika utoaji huduma za Bohari ya Dawa (MSD) kinachounganisha wateja, wadau na MSD, kwa ajili ya kupata huduma bora. Kitengo hiki huratibu na kusimamia shughuli za kila siku za mawasiliano na mahusiano ya wateja katika ofisi zote za kanda na kurugenzi, lengo likiwa ni kuboresha hali ya utoaji wa huduma, kuongeza kuridhika kwa wateja, na kuimarisha uhusiano na wadau wa MSD kote nchini.


Kitengo cha Huduma kwa Wateja pia kinasimamia na kuendesha jukwaa la kidijiti la mfumo wa taarifa za MSD (MSD Customer Portal), lililobuniwa ili kuwapatia wateja huduma na taarifa muhimu kwa urahisi, kwa wakati halisi, na kwa uwazi zaidi. 


Kupitia jukwaa hili la kidijiti (MSD Customer Portal), wateja wa MSD wanaweza kupata taarifa zifuatazo 
1.Kuangalia Hali ya Bidhaa ghalani: Kufuatilia upatikanaji wa dawa na bidhaa za afya zilizopo ghalani.
2.Kupata Orodha za Bei: Kupata bei za bidhaa zilizowasilishwa kwa ajili ya mipango na ununuzi.
3.Kufuatilia Oda: Kupata mwenendo wa oda zao kuanzia hatua ya kuagiza hadi kusafirishwa na kukabidhiwa.
4.Kuona Taarifa za Akaunti ya Mteja: Kupata taarifa na rekodi za miamala yao kwa urahisi.
5.Kusajili Malalamiko: Kuwasilisha na kufuatilia malalamiko au mrejesho kwa ajili ya kushughulikiwa haraka.


Baadhi ya majukumu mengine ya kitengo hiki ni pamoja na; Usajili wa Wateja Wapya, Usimamizi wa Miradi, Ushiriki katika Huduma za Jamii,  na Ushughulikiaji wa Malalamiko, ambapo ushauri, maswali, hoja au malalamiko yote yanayowasilishwa kupitia mfumo wa kielekrtoniki wa huduma kwa wateja wa MSD (Customer portal) au E-Mrejesho au kupitia namba ya bure ya huduma kwa wateja 0736 844 844, hufuatiliwa na kushughulikiwa na kitengo cha Huduma kwa Wateja ili kuhakikisha kila mteja anapewa mrejesho stahiki.


Kitengo hiki kimeiwezesha MSD kutoa huduma zenye uwajibikaji, uwazi, na mwelekeo wa kumjali mteja, hivyo kuimarisha dhamira yake ya ubora chini ya kaulimbiu isemayo: “Tumedhamiria Kuokoa Maisha.”
 

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.