Ruka kwenda maudhui makuu

Kitengo cha Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini


Kitengo cha Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini pia hujulikana kama Ofisi ya Usimamizi wa Kimkakati ni kitovu cha maarifa cha MSD kinachojishugulisha na  uchanganuzi wa utendaji kazi, utekelezaji wa Mpango mkakati , ubunifu kupitia uchanganuzi wa taarifa, udhibiti wa vihatarishi na kufanya tathmini utekelezaji wa majukumu ya MSD.


Kitengo cha Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini, kama kitovu cha maarifa cha taasisi huakikisha malengo, shughuli na rasilimali za MSD zinaendana na vipaumbele na malengo ya MSD ya muda mrefu. Kitengo hiki huratibu uandaaji na utekelezaji wa Mpango Mkakati, kufuatilia utekelezaji wake, utendaji kazi wa taasisi kwa kutumia viashirio muhimu vya  utendaji na kuipatia menejimenti taarifa ya kitaalamu inayowezesha kufanya  uamuzi sahihi. 


Pia, Kitengo cha Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini huratibu shughuli za utafiti, uchanganuzi wa uwekezaji na tathmini ya vihatarishi  ili kuhakikisha mpango mkakati  unasimamiwa na kutekelezwa kwa ufanishi. Kitengo hiki kina watalaamu mbalimbali kama vile wafamasia, wachanganuzi wa masuala ya fedha, wabobezi wa masuala ya mnyororo wa ugavi, watakwimu, wachumi, na wachanganuzi wa vihatarishi ambao kwa pamoja huisaidia taasisi kutoa huduma bora  na matokeo yanayopimika katika utekelezaji wa shughuli zake. 


Kwa kusimamia utamaduni wa utendaji kazi na uwajibikaji, Kitengo cha Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini huimarisha ufanisi, utawala bora, na ustahimilivu. Uongozi na utendaji  wake wa ufuatiliaji wa kimkakati na tathmini huhakikisha MSD  inaendelea  kutoa huduma bora, endelevu na za uhakika za mnyoro wa ugavi wa bidhaa za afya nchi nzima.
 

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.