Ruka kwenda maudhui makuu

Kitengo cha Mpango wa Soko la Ukanda


Kitengo cha Masoko ya Kanda kinapanua huduma za MSD nje ya mipaka ya Tanzania kwa kuimarisha ushirikiano wa kikanda na ununuzi wa bidhaa za afya kwa pamoja. Kupitia miundombinu ya kisasa na mifumo  iliyounganishwa ya TEHAMA, MSD inahakikisha bidhaa za afya zinapatikana maeneo yote.


Kwa kutambua uwezo wa kiutendaji wa MSD, Mawaziri wa Afya wa nchi wanachama   Jumuiya ya Mandeleo Kusini mwa Afrika (SADC), mwaka 2017 huko Polokwane, Afrika Kusini, waliipitisha MSD kuwa taasisi rasmi ya kufanya ununuzi wa pamoja wa bidhaa za afya kwa niaba ya nchi  kumi na sita (16)  wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika- SADC, zenye idadi ya watu takribani milioni 346.


Ili kuwezesha utekelezaji wa jukumu hilo, MSD iliunda Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Pamoja wa SADC (Electronic SADC Pooled Procurement System – eSPPS) unaoratibu shughuli za ununuzi kikanda kwa uwazi na ufanisi zaidi. Kitengo cha Masoko cha Kanda, kinashirikiana kwa karibu na nchi wanachama wa SADC kuanisha orodha za bidhaa za afya, kuoanisha orodha za bidhaa muhimu za kitaifa, na kudumisha ushirikiano endelevu wa kikanda katika mnyororo wa ugavi.


Nchi Wanachama wa SADC ni pamoja na Angola, Botswana, Comoros, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Eswatini, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Seychelles, Afrika Kusini, Tanzania. Zambia na Zimbabwe
 

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.