Ruka kwenda maudhui makuu

Kanda ya Iringa
Kanda ya MSD Iringa ilianzishwa rasmi tarehe 7 Aprili, 2004 kama moja ya kanda 10 za kiutendaji za MSD, ikianzishwa kimkakati kuhudumia mikoa ya nyanda za juu kusini mwa Tanzania. Kanda hii ilianzishwa chini ya mpango wa Serikali wa ugatuaji wa mamlaka kwa lengo la kuboresha usambazaji wa dawa na vifaa tiba. Uanzishwaji wake umechangia kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa huduma za afya za uhakika, hasa kwa jamii zilizo pembezoni, kwa kupeleka huduma karibu zaidi na jamii ili kuimarisha usawa na kusaidia utekelezaji wa dhamira ya nchi ya kujenga jamii yenye afya bora.
Kwa sasa, Kanda ya Iringa inahudumia jumla ya mikoa mitatu (3) ambayo ni Iringa yenyewe, Njombe na Ruvuma, isipokuwa Halmashauri za Wilaya ya Makete na Tunduru  zinahudumiwa na Kanda za Mbeya na Mtwara kutokana na ukaribu wa eneo la kijiografia.
 

Mawanda ya Utoaji Huduma
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi nchini Tanzania ya mwaka 2022, Kanda ya MSD Iringa inahudumia jumla ya watu 3,410,254. Idadi hii inajumuisha wakazi kutoka mikoa ifuatayo: 
Mkoa wa Iringa – watu 1,192,728, 
Mkoa wa Ruvuma – watu 1,436,740 (ukiondoa Wilaya ya Tunduru) na 
Mkoa wa Njombe – watu 780,786 (ukiondoa Wilaya ya Makete)
Kanda ya MSD Iringa inahudumia jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 930, ikijumuisha vituo kuanzia ngazi ya msingi, ngazi ya kati, hadi ngazi ya taifa.
1. Vituo ngazi ya kati na taifa – Hospitali za Rufaa za Mikoa 3.
2. Vituo ngazi ya msingi – Hospitali  18 za wilaya zilizo chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – (TAMISEMI), vituo vya afya 84, na zahanati 757.
3. Vituo vya Tasisi za kidini na taasisi nyingine za umma - Taasisi za dini 20 pamoja na taasisi nyingine za umma 48.
 

Uwezo wa Uhifadhi na Uendeshaji
Ili kuhudumia vituo vya afya ipasavyo na kwa ufanisi, kanda hii ina ghala lenye ukubwa wa eneo la mita za mraba 1,534 na magari 13 ya usambazaji yenye ukubwa tofauti kulingana na mahitaji. Rasilimali hizi kwa pamoja huiwezesha Kanda kutunza, na kusambaza dawa na vifaa tiba kwa ufanisi na kwa kuzingatia viwango vya juu vya ubora na usalama.
Mafanikio ya kanda ya MSD Iringa yanatokana na uwapo wa timu ya wataalamu 36 ikihusisha wabobezi wa masuala ya ugavi ,wafamasia, wahasibu, wawakilishi wa mauzo, maofisa huduma kwa wateja, mafundi sanifu vifaa tiba na madereva. Mchango wao wa kitaalamu  unahakikisha kuwa kanda hii inaendelea kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, hivyo kuboresha utoaji wa huduma za afya na kuongeza ufanisi wa usambazaji  katika maeneo yake.
 

Utoaji wa Huduma Bora
Kwa kuzingatia eneo lake la kimkakati, miundombinu ya kisasa, na nguvu kazi yenye ujuzi, Kanda ya MSD Iringa inaendelea kuwa mhimili muhimu katika kuboresha utoaji wa huduma za afya katika maeneo ya mikoa ya Kanda ya ziwa nchini Tanzania.
Kanda hii pia, inaendelea kujidhatiti kutekeleza dira kuu ya MSD ya kuwa "Kituo Bora cha Umahiri katika Mnyororo wa Ugavi wa Bidhaa za Afya Barani Afrika".
 

Location Map
36.20485484481565,-115.20025440468748

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.