Kitengo cha Miradi Misonge
Kitengo cha Miradi Msonge cha Bohari ya Dawa (MSD) ni kiini cha mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya nchini Tanzania, kikihakikisha uratibu na upatikanaji wa bidhaa za afya kwa ajili ya program za VVU/UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria, Chanjo, na Afya ya Uzazi na Mtoto.
Hapo kabla, programu hizi zilikuwa zikiendeshwa bila kushirikiana chini ya Wizara ya Afya, kila programu iliendesha mfumo wake wa ugavi, na kusababisha kukosa ufanisi na kuwa na matumizi ya rasilimali yasiyo na tija. Mwaka 1996, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliunganisha shughuli zote za ugavi kuwa chini ya MSD ili kurahisisha utendaji kazi, kupunguza gharama, na kuimarisha uwajibikaji katika mnyororo wa ugavi.
Kitengo hiki kinasimamia ununuzi, uhifadhi, na usambazaji wa bidhaa za programu kwa kushirikiana kwa karibu na wabia wakubwa wa maendeleo kama vile Mfuko wa Dunia, UNICEF, Shirika la Afya Duniani, na USAID. Ushirikiano wa programu unahakikisha bidhaa zinazogharamiwa na wahisani zinatolewa kwa wakati, uwazi, na kwa ufanisi katika vituo vya kutolea huduma za afya nchi nzima.
Kupitia uratibu thabiti, mifumo iliyounganishwa na kuzingatia viwango vya ubora, Kitengo cha Miradi Msonge za kinatekeleza dhamira ya MSD ya kuhakikisha kunakuwa na mnyororo wa ugavi bora, wenye ufanisi, kuamika na endelevu wa bidhaa za afya za miradi msonge nchini Tanzania.