Kitengo cha Uhakiki Ubora
Kitengo cha Udhibiti Ubora kina jukumu la kuhakikisha MSD inatoa huduma bora, zenye viwango na za uhakika nchi nzima. Kupitia ukaguzi wa ndani, tathmini za vihatarishi, na hatua za tahadhari za kiusalama, kitengo hiki husaidia kuhakikisha huduma za MSD zinaendelea kutolewa licha ya changamoto zinazoweza kujitokeza.
Bohari ya Dawa (MSD) ina Mfumo wa Udhibiti Ubora (QMS) uliothibitishwa kwa viwango vya ithibati ya kimataifa ya ubora, yaani ISO 9001:2015, ikiashiria dhamira ya taasisi ya kuhakikisha inatoa huduma bora, kwa wakati na kwa ufanisi. Mifumo ya udhibiti ubora na taratibu za uendeshaji hufanyiwa tathmini, ukaguzi, na maboresho ya mara kwa mara ili kuhakikisha taasisi inatoa huduma ubora, endelevu na zinazokidhi viwango vya kimataifa.
Mfumo huu wa udhibiti ubora unahusika na udhibiti thabiti wa taratibu za uendeshaji, usimamizi wa mabadiliko, udhibiti vihatarishi, kushughulikia upungufu, na uchanganuzi wa taarifa. Hatua hizi zinachangia kuleta uadilifu na ufanisi wa uendeshaji shughuli za MSD katika maeneo ya uhifadhi bidhaa za afya, huduma kwa wateja, takwimu muhimu, TEHAMA, rasilimaliwatu,na usimamizi wa usalama.
Juhudi hizi za maboresho endelevu pamoja na programu za mafunzo ya ndani zimesaidia kujenga utamaduni wa utendaji kazi katika vituo vyote vya MSD.