Kanda ya Tanga
Kanda ya MSD Tanga ilianzishwa mwaka 2015 kama Kituo cha Mauzo chini ya Kanda ya Kilimanjaro (awali ikijulikana kama Kanda ya Moshi). Kituo hicho kilipandishwa hadhi mwaka 2019 na kuwa Ofisi Kamili ya Kanda ili kuimarisha utoaji wa huduma za afya na kupanua wigo wake. Tangu wakati huo, Kanda hii imekuwa kitovu muhimu cha mtandao wa ugavi wa MSD, ikiwa na jukumu la kimkakati kaskazini mwa Tanzania. Kanda ya MSD Tanga inahudumia Mkoa wa Tanga ukiwa na Wilaya 11, pamoja na Wilaya ya Same kutoka Mkoa wa Kilimanjaro (ukaribu wa kijiografia na urahisi wa usambazaji.)
Mawanda ya Utoaji Huduma
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi nchini Tanzania ya mwaka 2022, Kanda ya Tanga inahudumia jumla ya watu 2,915,900. Idadi hii inahusisha:
Mkoa wa Tanga - Wilaya ya Kilindi – watu 398,391,
Halmashauri ya Jiji la Tanga – watu 393,429,
Wilaya ya Handeni (Vijijini) – watu 384,353,
Wilaya ya Lushoto – watu 350,958,
Wilaya ya Korogwe (Vijijini) – watu 272,870,
Wilaya ya Muheza – watu 238,260,
Wilaya ya Bumbuli – watu 159,373,
Wilaya ya Mkinga – watu 146,802,
Halmashauri ya Mji wa Handeni – watu 108,968,
Halmashauri ya Mji wa Korogwe – watu 86,551,
Wilaya ya Pangani – watu 75,642 na
Mkoa wa Kilimanjaro (Wilaya ya Same) – watu 300,303)
Kanda ya MSD Tanga hivi sasa inahudumia jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 612, ikijumuisha vituo kuanzia ngazi ya msingi, ngazi ya kati, hadi ngazi ya taifa.
1. Vituo ngazi ya kati na taifa – Hospitali ya Rufaa ya Mikoa 1, na hospitali bobezi 1
2. Vituo ngazi ya msingi – Hospitali 12 za wilaya zilizo chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – (TAMISEMI), vituo vya afya 43, zahanati 528,
3. Vituo vya Tasisi za kidini na taasisi nyingine za umma - Taasisi za dini 5, na taasisi nyingine za umma 25.
Uwezo wa Uhifadhi na Uendeshaji
Ili kuhudumia idadi kubwa ya vituo vya afya ipasavyo na kwa ufanisi, kanda hii ina ghala lenye ukubwa wa eneo la mita za mraba 4,218 na magari 12 ya usambazaji yenye ukubwa tofauti kulingana na mahitaji. Rasilimali hizi kwa pamoja huiwezesha Kanda hii kutunza, na kusambaza dawa na vifaa tiba kwa ufanisi na kwa kuzingatia viwango vya juu vya ubora na usalama.
Mafanikio ya kanda ya MSD Tanga yanatokana na uwapo wa timu ya wataalamu 31 ikihusisha wabobezi wa masuala ya ugavi ,wafamasia, wahasibu, wawakilishi wa mauzo, maofisa huduma kwa wateja, mafundi sanifu vifaa tiba na madereva. Mchango wao wa kitaalamu unahakikisha kuwa kanda hii inaendelea kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, hivyo kuboresha utoaji wa huduma za afya na kuongeza ufanisi wa usambazaji katika maeneo yake.
Utoaji wa Huduma Bora
Kwa kuzingatia eneo lake la kimkakati, miundombinu ya kisasa, na nguvu kazi yenye ujuzi, Kanda ya MSD Tanga inaendelea kuwa mhimili muhimu katika kuboresha utoaji wa huduma za afya katika maeneo ya kaskazini mwa Tanzania.
Kanda hii pia, inaendelea kujidhatiti kutekeleza dira kuu ya MSD ya kuwa "Kituo Bora cha Umahiri katika Mnyororo wa Ugavi wa Bidhaa za Afya Barani Afrika".