Ruka kwenda maudhui makuu

Kanda ya Kagera
Kanda ya MSD Kagera ilianzishwa mwaka 2013 kama kituo cha mauzo chini ya Kanda ya Mwanza, na baadae mwaka 2021 kilipandishwa hadhi kuwa kanda  kamili inayojitegemea. Kanda ya Kagera ipo katika pembe ya kaskazini magharibi mwa Tanzania Bara, ikiwa na  jukumu muhimu la kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya,  katika Mkoa wa Kagera na katika  halmashauri tatu za Mkoa wa Geita ambazo ni Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, Halmashauri ya Wilaya ya Chato, na Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe.
 

Mawanda ya Utoaji Huduma
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Kanda ya Kagera ya MSD, inahudumia jumla ya watu 4,344,219. Mchanganuo huo ni kama ifuatavyo.
Mkoa wa Kagera - watu 2,989,299.
Mkoa wa Geita - Halmashauri ya Mbogwe watu 362,855, 
Wilaya ya Chato watu 584,963, na 
Wilaya ya Bukombe watu 407,102.
Kwa ujumla Kanda ya Kagera inahudumia jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 477, ikijumuisha vituo kuanzia ngazi ya msingi, ngazi ya kati, hadi ngazi ya taifa.
1. Vituo ngazi ya kati na taifa – Hospitali 1 ya Rufaa ya Kanda, na hospitali 1 ya Rufaa ya Mkoa.
2. Vituo ngazi ya msingi – Hospitali  11 za wilaya zilizo chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – (TAMISEMI), hospitali teule 6 za wilaya, vituo vya afya 53, na zahanati 341.
3. Vituo vya Tasisi za kidini na taasisi nyingine za umma - Taasisi za dini 5, na taasisi nyingine 59.

Uwezo wa Uhifadhi na Uendeshaji
Ili kuhudumia vituo vya afya ipasavyo na kwa ufanisi, kanda hii ina ghala lenye ukubwa wa eneo la mita za mraba 2,700 na magari 13 ya usambazaji. Rasilimali hizi kwa pamoja huiwezesha Kanda kuhifadhi, na kusambaza dawa na vifaa tiba kwa ufanisi kwa kuzingatia viwango vya juu vya ubora na usalama.
Kwa ujumla, Mafanikio ya kanda ya Kagera yanatokana na uwapo wa timu ya wataalamu 26 ikihusisha wabobezi wa masuala ya ugavi, wafamasia, wahasibu, wawakilishi wa mauzo, maofisa huduma kwa wateja, mafundi sanifu vifaa tiba na madereva. Mchango wao wa kitaalamu unahakikisha kuwa kanda hii inaendelea kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, hivyo kuboresha utoaji wa huduma za afya na kuongeza ufanisi wa usambazaji  katika maeneo yake.
 

Utoaji wa Huduma Bora
Kwa kuzingatia eneo lake la kimkakati, miundombinu ya kisasa, na nguvu kazi yenye ujuzi, Kanda ya MSD Kagera inaendelea kuwa mhimili muhimu katika kuboresha utoaji wa huduma za afya katika mikoa ya Kandaa ya kati nchini Tanzania.
Kanda hii inaendelea kujidhatiti kutekeleza dira kuu ya MSD ya kuwa "Kituo Bora cha Umahiri katika Mnyororo wa Ugavi wa Bidhaa za Afya Barani Afrika."

 

Location Map
36.20485484481565,-115.20025440468748

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.