Skip to main content
Baadhi ya Viongozi wa Serikali ya Tanzania, SADC na Wadawau Mbalimbali Wakiwa Kwenye Picha ya Pamoja

SADC Yazindua Kanzidata ya Mfumo wa Taarifa za Bidhaa za Afya Kwa Nchi Wanachama.

Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) imezindua Kanzidata maalumu kwaajili ya ukusanyaji na uchakataji wa taarifa za Dawa na vifaa tiba kutoka kwa wazalishaji na wazabuni mbalimbali Duniani, ambapo mfumo huo utarahisisha upatikanaji na ununuzi wa bidhaa za afya kutoka kwa nchi wanachama.

Uzinduzi huo umefanyika tarehe 14/05/2024 jijini Dar es salaam, na kushuhudiwa na Bohari za Dawa za nchi za SADC, pamoja na viongozi mbalimbali wa Sekta ya Afya wa jumuiya hiyo, ambao walikutana kwa siku mbili jijini humo.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu amesema kupitia mfumo utawawezesha nchi wanachama kupata taarifa za kina juu ya Dawa na vifaa tiba kama vile sehemu zinavyopatikana ama kutengezewa, bei, pamoja na kujua muda wa bidhaaa husika kuharibika,.

Ameongeza kuwa hatua hiyo inasaidia kufikia adhima ya Viongozi wa kuu wa Nchi za SADC wa kuwa na mfumo wa manunuzi ya pamoja ya bidhaa za Afya kwani wanaponunua kwa pamoja hupunguza gharama, pia kuaongeza nguvu ya kiushawishi na kuvutia wawekezaji kufungua viwanda vya dawa na vifaa tiba ndani ya Nchi za SADC.

“Mfumo huu ni nyenzo muhimu katika sekta ya Afya wa kuhamasisha ushirikiano miongoni mwa nchi za SADC katika Afya za watu wetu hivyo madawa na vifaa tiba ni muhimu katika kulinda Afya ya Binadamu “Amesema Dkt. Jingu.

Kwa upande wake mwakilishi wa sekretarieti ya SADC Calicious Tutalife amesema SADC kupitia mfumo huo wataweza kubadilishana taarifa muhimu hususani za ununuzi wa pamoja na kufanya maamuzi ya bidhaa gani wanunue ili kubunguza gharama na kuongeza ufanisi.

Aidha amesema watatumia mfumo huo kupata bidhaa bora na nafuu kupitia taarifa watakazozipata kwenye mfumo na kutengeneza mpango ambao watausimamia.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Tanzania Tukai Mavere amesema Kanzi data hiyo itatumika kutunza taarifa za bidhaa za Afya, nchi inakotoka, ubora wake, gharama yake ambapo itasaidia watu kujua nchi tofauti zinapataje bidhaa zake na bei.

Hata hivyo amesema ili kuhakikisha kunakuwepo na ufanisi, kitaundwa kitengo maalum cha pamoja, ambacho kitakuwa na bodi ya usimamizi kutoka nchi wanachama, kwani jukumu hilo ni la kimataifa.

Ameongeza kuwa hivi sasa MSD kwa kushirikiana na Sekretarieti ya SADC watafanya mapitio ya bidhaa za afya zinazohitajika, na wataangalia sheria, miongozo, pamoja na kupata vibali vyote vya serikali kwa nchi wanachama, kwani ni maeneo muhimu katika kutekeleza ununuzi wa pamoja.

Itakumbukwa kuwa Tanzania Ndio nchi iliyochaguliwa na SADC kutekeleza jukumu la ununuzi wa Pamoja wa dawa na vifaa tiba vya nchi zote za SADC kupitia MSD, kutokana na Tanzania kuonekana kufanya vizuri katika eneo hilo.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.