MSD yaendelea kutoa elimu kupitia maonyesho
Bohari ya Dawa (MSD) inashiriki katika maonesho ya kimataifa ya bidhaa za Afya (Medexpo) yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Lengo la maonyesho hayo ni kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya afya kutoka ndani na nje ya nchi.
MSD ikiwa mmoja wa wadau wakubwa kwenye sekta ya afya inashiriki maonesho hayo kwa kutoa elimu kwa wadau kuhusu namna ya kushiriki kwenye zabuni zinazotangazwa na MSD kupitia mfumo wa Nest, pamoja na kuwajengea uelewa wadau juu ya sheria na taratibu za ununuzi wa umma.
Aidha, wananchi na wadau mbalimbali wa MSD wamepata wasaa wa kujionea bidhaa za afya mbalimbali zinazozalishwa na zinazosambazwa na MSD kwenye vituo vya kutolea hufuma za afya. Bidhaa hizo ni pamoja na vifaa tiba, dawa na vitendanishi vya maabara.