Skip to main content
wishega

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala MSD, Ahimiza Watumishi Kutimiza Majukumu Yao

"Hakuna Haki Bila Wajibu" – Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala MSD, Ahimiza Watumishi Kutimiza Majukumu Yao. 

Katika kuendeleza uwajibikaji na ufanisi mahali pa kazi, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Mboyi Wishega, ametoa wito kwa watumishi wa taasisi hiyo kuzingatia wajibu wao kikamilifu ili kustahili haki zao zinazotolewa kwa mujibu wa taratibu na sheria za utumishi wa umma.

Akizungumza katika kikao kazi na madereva wa MSD, Bw. Wishega alisisitiza kuwa haki na wajibu ni dhana zinazokwenda pamoja, na kwamba haitarajiwi mtumishi kudai haki bila kutimiza wajibu wake ipasavyo.

"Hakuna haki bila wajibu! Hivi ni vitu viwili vinavyokwenda sambamba. MSD imeendelea kuwapatia watumishi wake haki zao kwa mujibu wa sheria, hivyo ni wajibu wa kila mtumishi kuhakikisha anatimiza majukumu yake kwa uadilifu na weledi," alieleza Bw. Wishega.

Katika kikao hicho, kilicholenga kuhimiza uwajibikaji, nidhamu, na kutoa mrejesho kuhusu utendaji wa kazi, Bw. Wishega aliwataka madereva kuwa mfano wa kuigwa kwa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia kanuni za usalama barabarani, utunzaji wa vyombo vya usafiri, pamoja na kuheshimu muda na maadili ya kazi.

Aidha, aliwahakikishia watumishi hao kuwa MSD itaendelea kuboresha mazingira ya kazi na kutoa haki zote stahiki ikiwa ni pamoja na mafao, likizo, bima za afya, na fursa za mafunzo – ilimradi wajibu pia utekelezwe kwa kiwango kinachotarajiwa.

Add new comment

Restricted HTML

  • You can align images (data-align="center"), but also videos, blockquotes, and so on.
  • You can caption images (data-caption="Text"), but also videos, blockquotes, and so on.

About

MSD was established for the purpose of production, procurement, storage, and distribution of approved health commodities required for use by health facilities. In living this mission, we ensure that health commodities in Tanzania are accessible, reliable, and affordable but also delivered on time at all health facilities in Tanzania and beyond.

Featured Posts

Contact info

Our mission: To make quality health products accessible to all public health facilities in Tanzania.