Skip to main content

Katibu Tawala Dar es Salaam apongeza MSD kwa utekelezaji bora


Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Abdul Mhinte, ameipongeza Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Dar es Salaam kwa utekelezaji mzuri wa majukumu yake, huku akitoa wito kwa watendaji wa sekta ya afya mkoani humo kuhakikisha wanadhibiti na kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kuwezesha ulipaji wa madeni kwa wakati.

Akizungumza leo, Septemba 17, 2025, jijini Dar es Salaam wakati wa kufungua kikao cha wateja na wadau wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, Mhinte amesema kuwa usimamizi mzuri wa mapato yatokanayo na huduma za afya ni muhimu katika kuhakikisha vituo vinaweza kununua bidhaa muhimu na kusimamia vyema mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya.

Aidha, amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuongeza bajeti ya ununuzi wa bidhaa za afya ili kuboresha huduma kwa wananchi.

Mhinte ameongeza kuwa uwepo wa kikao hicho ni chachu ya kutoa uelewa zaidi kuhusu mifumo ya MSD, kubadilishana uzoefu na kujadili namna bora ya kushirikiana ili kuboresha utoaji wa huduma za afya.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ugavi na Uendeshaji wa MSD, Victor Sungusia, amesema kuwa serikali imeongeza bajeti ya dawa kutoka Shilingi bilioni 200 hadi bilioni 300 kwa mwaka, ikiwa ni sehemu ya kuboresha huduma za afya nchini.

“Tunaendelea kuboresha utendaji kazi wetu, kuhakikisha huduma inapatikana kwa wakati. Naomba washiriki wa kikao hiki mtoe mrejesho ili tuweze kuboresha zaidi,” amesema Sungusia.

Naye Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, Betia Kaema, amesema kuwa MSD inajenga mfumo madhubuti wa ununuzi, utunzaji na usambazaji wa bidhaa za afya kwa kutumia mbinu na ushauri wa kitaalamu.

Ameongeza kuwa upatikanaji wa bidhaa za afya umeongezeka kutoka asilimia 54 katika mwaka wa fedha 2023/24 hadi asilimia 74, na wanatarajia kufikia asilimia 90 katika mwaka wa fedha 2025/26

Add new comment

Restricted HTML

  • You can align images (data-align="center"), but also videos, blockquotes, and so on.
  • You can caption images (data-caption="Text"), but also videos, blockquotes, and so on.

About

MSD was established for the purpose of production, procurement, storage, and distribution of approved health commodities required for use by health facilities. In living this mission, we ensure that health commodities in Tanzania are accessible, reliable, and affordable but also delivered on time at all health facilities in Tanzania and beyond.

Featured Posts

Contact info

Our mission: To make quality health products accessible to all public health facilities in Tanzania.