Skip to main content

Wataalamu wa Afya Kutoka Sierra Leone, Wafanya Ziara ya Mafunzo MSD

Wataalamu wa Afya kutoka nchini Sierra Leone leo wametembelea Bohari ya Dawa (MSD) kwa lengo kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu shughuli za Ugavi, Uhifadhi, Uendeshaji, Ununuzi, Huduma kwa Wateja, Sera, Udhibiti Ubora, pamoja na mambo mengine yanayohusu mnyororo wa Ugavi wa bidhaa za afya.

Akiongea kwa niaba ya Wizara ya Afya wakati wa kuukaribisha ujumbe huo nchini, Mfamasia Mkuu wa Serikali Daudi Msasi, amesema ujio wa wageni hao ni ishara kwamba kama nchi tumeboresha na kuimarisha Bohari yetu katika utoaji wa huduma, ndio maana wengine wanakuja kujifunza.

Amesema Tanzania ipo tayari kuwapa ushirikiano wa kutosha kwa maslahi mapana ya wananchi wa Afrika.

“Ukiona mtu amechambua nchi mbalimbali, akaja kajifunza Tanzania inamaanisha tunafanya vizuri na ndio maana ndugu zetu hawa wakachagua kuja hapa kujifunza, hivyo ni ugeni mzito ambao umeongozwa na Mganga mkuu wa nchi yao”.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai, amebainisha kwamba kutokana na mabadiliko ya kiutendaji, MSD imeendelea kuvutia wengi kuja kujifunza na kuimarisha mnyororo wa Ugavi wa bidhaa za afya katika nchi zao.

“Tunakumbuka Sierra Leon ni nchi ambayo ilikubwa na matatizo ya amani ambayo yalivunja vunja mfumo mzima wa afya na sasa wameamka na kujikung’uta na kuanza upya mfumo wao wa afya na sasa wamekuja huku kujifunza namna ya sisi tunavyofanya kazi zetu.

Amesema moja ya kitu kilichowavutia zaidi ni ubunifu ambao MSD wamekuwa nao katika kufanya shughuli zao za kuzalisha, kununua, kutunza na kusambaza dawa lakini pia uhimilivu wa kifedha sambamba na matumizi ya Tehama.

Aidha ameongeza kuwa kupitia ziara hiyo, wamejadiliana jinsi Bohari ya Dawa ya Sierra Leone inavyoweza kushirikiana na wadau wengine ndani ya serikali na nje ya serikali ikiwemo kuunganisha mifumo yao na idara mbalimbali, kama fedha, utumishi, wateja, na wizara ya afya ya nchi hiyo, ili kuwa na mnyororo wa Ugavi imara na endelevu wa Bidhaa za afya.

Kwa upande mmoja wa viongozi waliombatana na ujumbe huo, ambaye ni Mfamasia Mkuu wa Sierra Leone Dkt. Moses Batema amesema kabla ya ujio huo wamefanya utafiti wa kutosha na kuona sehemu ya kwenda kujifunza ni Tanzania hivyo wameridhishwa na majadiliano walioyafanya lakini pia wamejifunza vitu vingi vitakavyowasaidia kuboresha Bohari yao.

Ujumbe huo kutoka Sierra Leone ulioko nchini kwa ziara ya siku 4, chini ya uenyeji wa MSD, unajumuisha Mganga Mkuu (Wizara Ya Afya SL), Mfamasia Mkuu (WAF-SL), Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya NMSA ambayo ina majukumu kama MSD, Mkurugenzi Mkuu NMSA, Msajili wa Bodi ya wafamasia (SL), Mkuu wa Ugavi (WAF SL), Mkurugenzi wa Ununuzi (NMSA), Mkurugenzi wa Ugavi (NMSA), baadhi ya watumishi kutoka Global Fund na UNFPA kutoka nchini SL

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.