MSD yafanya kikao na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC),
Bohari ya Dawa (MSD) leo imefanya kikao muhimu na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Mheshimiwa Elias M. Magosi, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa SADC, kikao hiko kiliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai, kilikuwa na lengo la kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika sekta ya afya.
Katika kikao hicho, pande zote mbili zilijadiliana kuhusu mikakati ya pamoja ya kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya ndani ya ukanda wa SADC, kuongeza usalama wa bidhaa za afya, pamoja na kushirikiana katika maeneo ya uzalishaji, utafiti, na usambazaji wa dawa.