Skip to main content
  • Bidhaa za Mama na Mtoto

    Hadi kufikia mwaka 2025 MSD tayari imekamilisha ununuzi na usambazaji wa vifaa tiba vya kupambana na vifo vya uzazi pingamizi CEmONC kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. MSD imeweza kufanya ununuzi wa vifaa tiba vyenye thamani ya Tzs. 100,182,390,897.40 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya 414. Katika vifaa tiba hivi asilimia themanini (80) imejikita katika vifaa vya upasuaji kama taa za upasuaji, mashine za usingizi, vitanda vya upasuaji ambavyo vimeenda okoa Maisha ya wamama na Watoto nchini Tanzania.

  • Mifumo yetu ya TEHAMA sasa inasomana

    MSD ilipoanzishwa, majukumu yake ya ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za Afya yalikuwa yakifanyika bila kutumia mifumo ya TEHAMA  ambapo watumishi walitumia makarasi maalum yaliyotumika kuagiza na kuhifadhi kumbukumbu ya bidhaa za afya kama Bin Card, Combined Requisition and Issue note (CRIN) . Mnamo mwaka 1998 matumizi ya TEHAMA yalianza kutumika katika kuimarisha utendaji wa majukumu yake katika eneo la usimamizi wa fedha kwa kutumia mfumo ulioitwa Navision Financials.

  • Bodi ya Wadhamini MSD, Yaridhishwa Usambazaji wa Vifaa Tiba Kuwezesha Uzazi Pingamizi kwa Mama na Mtoto

    Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini MSD Dkt. Ritah Mutagonda, ambaye amefanya ziara kwa wateja wanaohudumiwa na Kanda ya Kilimanjaro, amefurahishwa na utekelezaji wa usambazaji wa vifaa vya kisasa vya kuwezesha uzazi pingamizi kwa mama na mtoto.

    Mjumbe huyo ea Bodi ameyasema hayo walipotembelea kituo cha afya Uru Kyaseni, ambapo pamoja na mambo mengine amesema kwa serikali kupitia MSD  kuwezesha usambazaji wa vifaa hivyo kunapunguza idadi ku wa ya wagonjwa kufuata huduma hizo hospitaki ya Wilaya na ya rufaa ya mkoa.

  • MSD Yapongezwa kwa Maboresho ya Huduma Zake Mkoani Kagera

    Bohari ya Dawa (MSD) imepongezwa kwa kuimarisha mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya mkoani Kagera, ambao umepunguza malalamiko ya upungufu wa bidhaa za afya mkoani humo.

    Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa huo Steven Nashauri Ndaki, wakati akizungumza na ujumbe maalum kutoka MSD uliomtembelea ofisini kwake,  ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Bi. Rosemary Silaa, ikiwa ni ziara maalum ya kuadhimisha miaka 30 ya MSD.

  • MSD Yakabidhi Vifaa vya Upasuaji Vyenye Thamani ya Milioni 210 - Itigi

    Bohari ya Dawa (MSD) kupitia Kanda ya Dodoma  leo imekabidhi vifaa vya  upasuaji kwa hospitali ya Wilaya ya Itigi, iliyoko mkoani Singida, vyenye thamani ya jumla ya shilingi milioni 210.

    Akipokea vifaa hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Dkt.Vicent Mashinji amesema nia ya serikali kununua vifaa hivyo ni kuhakikisha huduma za afya zinatolewa kwa viwango vinavyokubalika, na kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika hasa kwa mama na watoto wakati wa kujifungua.

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.