Skip to main content
  • RMO Manyara - Avitaka Vituo vya Kutolea Huduma za Afya Kulipa Madeni ya MSD

    Watendaji kwenye vituo vya kutolea huduma za afya waliopo kwenye Mkoa wa Manyara wamekumbushwa kuendelea na utaratibu wa kulipa madeni ya Bohari ya dawa (MSD) kwani kufanya hivyo ni kuiwezesha MSD kuwa na mtaji mzuri wa kuendelea kununua bidhaa za afya ambazo zinasambazwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini. 

    Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt. Andrew Method alipokuwa  anafungua kikao cha wadau na wateja wa MSD kanda ya Kilimanjaro wa mkoani wa Manyara.  

  • MSD Kuimarisha Upatikanaji wa  Bidhaa za Maabara Nchini

    Bohari ya Dawa (MSD) imeadhimia kuboresha hali ya upatikanaji wa bidhaa za maabara nchini, ili kuimarisha uchunguzi wa vimelea vya magonjwa mbalimbali nchini.

    Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya (MSD) Rosemary Silaa, wakati alipotembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa - Bukoba na hospitali ya Wilaya ya Bukoba vijijini, ziara iliyolenga kupokea mrejesho wa huduma za MSD kutoka kwa wateja, ikiwa ni maadhimisho ya Miaka 30 toka MSD kuanza kazi zake rasmi.

  • Mkuu wa Wilaya ya Igunga Apongeza Maboresho ya Huduma za MSD

    Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe. Sauda Salum Mtondoo ameipongeza Bohari ya Dawa MSD kwa maboresho ya huduma zake, hali ilipelekea upatikanaji wa uhakika wa bidhaa za afya nchini, hivyo kuleta unafuu wa huduma kwa watoa huduma na wananchi kwa ujumla wilayani humo.

  • Ujumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Watembelea Kanda ya Kilimanjaro

    Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini MSD Dkt. Ritah Mutagonda, ambaye pia ni mlezi wa MSD Kanda ya Kilimanjaro ameipongeza Kanda ya MSD Kilimanjaro kwa kuvuka lengo la mauzo kwa kufikia 115% katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2024/2025.

    Mjumbe huyo wa Bodi ya Wadhamini ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake kwa wateja wanaohudumiwa na Kanda ya Kilimanjaro, kama moja ya shughuli za kuadhimisha miaka 30 ya utendaji wa MSD.

  • Wateja wa MSD Kanda ya Tanga Wapongeza Maboresho ya Huduma za MSD

    Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Tanga wameipongeza MSD kwa maboresho makubwa inayoendelea kuyafanya ya usambazaji wa bidhaa za afya kwa wakati.

    Pongezi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD ambaye pia ni Mlezi wa MSD  kanda hiyo, Dkt. Rukia Mwifunyi anayoifanya mkoani humo, kuzungumza na wateja wanaowahudumia ili kupata maoni yao juu ya huduma za MSD na kupokea changamoto zao ili ziweze kufanyiwa kazi.

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.