Skip to main content
  • Ujumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Watembelea Hospitali za Mkoa wa Simiyu

    Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Bw. Ally Seleman, akiambatana na Kaimu Meneja Mipango,Tathimini na Ufuatiliaji leo tarehe 20/11/24 wametembelea Kanda ya MSD Mwanza na kujionea jinsi Kanda hiyo inavyotekeleza majukumu yake,  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa MSD.

    Kupitia ziara hiyo Bw. Selemani amepokea taarifa ya utendaji wa Kanda hiyo, sambamba na mipango mbalimbali ambayo Kanda hiyo imejiwekea Ili kuhakikisha inaboresha huduma zake.

  • Ujumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Watembelea Kanda ya Mbeya

    Mwakilishi wa wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Bohari ya Dawa (MSD), Dr. Alex Magesa, ambaye alifuatana na Mkurugenzi wa Ununuzi Hamis Mpinda wamefanya ziara katika Kanda ya MSD, Mbeya, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa MSD.

    Katika ziara hiyo  viongozi  hao walitembelea wateja wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya na kuzungumza nao kuweza kujua namna wanavyozipokea huduma za MSD na kujadili kwa pamoja namna ya kuboresha huduma hizo.

  • Wanamichezo wa MSD Watoa Msaada wa Kijamii Kituo cha Afya Ngamiani

    Wanamichezo wa Bohari ya Dawa (MSD) wanaoshiriki kwenye mashindano ya SHIMUTA 2024 mkoani Tanga wametumia siku ya leo ya mapumziko kutembelea Kituo cha afya Ngamiani kilichopo mkoani Tanga na kutoa msaada wa bidhaa za afya kwa Wodi ya mama na mtoto. 

  • MSD Yatunukiwa Tuzo na Shule ya Famasia (MUHAS)

    Shule ya Famasia (MUHAS) imeitunuku Bohari ya Dawa (MSD) tuzo ya uhusiano mzuri wa kiutendaji pamoja ma ushirikiano.Tuzo hiyo imetolewa katika maadhimisho ya miaka 50 ya Shule hiyo na  kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD Ndg. Mavere Tukai kwa niaba ya watumishi wa MSD.

    Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Ndg. Mavere amesema MSD ni mdau wa shule ya famasia na imekua ikitoa ushirikiano kutoa mafunzo ya nadharia kwa wanafunzi katika ngazi mbalimbali. 

  • MSD Yashiriki Michuano ya SHIMUTA 2024

    Wachezaji wa Bohari ya Dawa (MSD) watakaoshiriki kwenye mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma,Taasisi na Makampuni Binafsi (SHIMUTA)  mwaka 2024 jijiniTanga, leo Ijumaa tarehe 8 Novemba 2024 wameagwa na Menejimenti ya MSD na kuanza safari ya kuelekea kwenye mashindano hayo. 

    Akizungumza wakati wa kuwaaga wachezaji hao Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Elisamehe Macha amewakumbusha watumishi hao kuwa michezo ni sehemu ya kazi hivyo wanapaswa kuhakikisha wanaenzi tunu za MSD ikiwemo uhodari na nidhamu kama wanapokuwa sehemu zao za kazi. 

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.