Skip to main content
  • MSD Yateta na Wazalishaji, Wasambazaji na Washitiri wa Bidhaa za Afya.

    Bohari ya Dawa (MSD) imekutana na wazalishaji, wasambazaji na washitiri wa bidhaa za afya zaidi ya 200 kutoka nje na ndani ya nchi kujadiliana namna ya kuboresha ushirikiano na kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya nchini.

    Katika hafla hiyo Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amewaeleza wadau hao kuwa serikali inaendelea kuboresha ushirikiano na sekta binafsi kuchagiza uanzishaji wa viwanda vya bidhaa za afya nchini.

    Nia kubwa ni kupunguza matumizi ya fedha za kigeni kununua bidhaa za afya kutoka nje ya nchi, ambapo kwa sasa asilimia 85 ya bidhaa hizo zinatoka nje ya nchi.

  • MSD Mfano wa Kuigwa SADC

    Wakuu wa Taasisi za Bohari ya Dawa pamoja na viongozi wanaosimamia manunuzi ya bidhaa za afya katika  Jumuia ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wameeleza kuwa Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) imekuwa mfano wa kuigwa katika nchi za jumuiya hiyo.

    Aidha wamesema MSD itakuwa chachu ya kuunganisha maendeleo na kukuza uchumi wa Afrika kutokana na ufanisi wake katika  upatikanaji wa uhakika wa dawa na bidhaa za afya.

  • Wafamasia na Wataalamu wa Maabara Nchini, Waaswa Kuzingatia Wajibu Wao

    Wafamasia na Wataalamu wa Maabara Kanda ya Kagera wametakiwa kutambua moyo wa sekta ya afya uko katika upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na kwamba kuhakikisha bidhaa hizo hazikosi katika vituo vya kutolea huduma.

    Hayo yamesemwa na Mganga mkuu wa Hospitali ya mkoa wa Geita Omary Sukari kwenye kikao cha majadiliano cha hali ya upatikanaji wa bidhaa za Afya kwa kanda ya kagera inayojumuisha wilaya ya Saba za mkoa kagera na wilaya tatu za Geita.

  • MSD Kuja na Suluhu ya Special Procurement

    Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD, ambaye pia ni mlezi wa Kanda ya MSD Kagera Bi. Rosemary Slaa, amewahakikishia wataalamu wa afya kutoka Mikoa ya Kagera na Geita kuwa Bohari ya Dawa (MSD) inaendelea kufanya maboresho katika upatikanaji wa bidhaa za afya nchini, mathalani upatikanaji wa vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa wakati.

  • MSD na Wadau wa Afya Mkoa wa Dar es Salaam Wahimizwa Kushirikiana

    Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Bi.Rehema Madenge, amewataka wadau wa afya mkoani humo, kushirikiana kwa karibu na Bohari ya Dawa (MSD) ili kuboresha huduma na kutatua changamoto mbalimbali zinazoukabili mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya mkoani humo. 

    Bi. Madenge ametoa rai hiyo hii leo, wakati akifungua kikao kazi baina ya Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Dar es Salaam na wadau wake wa afya mkoani humo, waliokutana kwa lengo la kujadili namna bora ya kuboresha mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya, huduma na mahusiano baina ya pande hizo mbili.

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.