Skip to main content
  • Dkt. Philip Mpango Aweka Jiwe la Msingi Kiwanda cha Mipira ya Mikono cha MSD, Kilichopo Idofi Makambako Mkoani Njombe

    Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amesema serikali inatambua vita iliyopo katika ujenzi wa viwanda vya dawa lakini kwa kuwa uwamuzi huo ni wa Rais Dk. Samia Suluhi Hassan hakuna atakayefanikiwa kuvikwamisha hivyo vitajengwa.

    Amesema kwa sasa  serikali inaagiza dawa kwa asilmia 80 na vifaa tiba kwa asilimia 90 kutoka nje ya nchi, hali inayosababisha uhaba wa vifaa na gharama kubwa za uagizaji wa vifaa vya afya  hivyo ni lazima kuchukua maamuzi magumu.

  • Rais Dkt. Samia Analeta Mapinduzi Viwanda vya Dawa

    WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu, amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amedhamiria kuleta mapinduzi katika sekta ya viwanda hasa vya dawa, vifaa tiba.

    Rais Dkt. Samia ameendelea kutoa fedha za uwekezaji katika sekta ya viwanda na miradi yote ya maendeleo iliyoanzishwa awamu ya tano inatekelezwa.

    Mwalimu aliyasema hayo mkoani Njombe wakati akikagua uzalishaji katika kiwanda cha mipira ya mikono (gloves) kilichopo Idofi, mkoani humo.

  • Upatikanaji wa Dawa nchini, Wapaa hadi Kufikia 81%

    Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa nchini (MSD), Mavere Tukai amesema kuwa upatikanaji wa dawa nchini umefikia asilimia 81 mwezi Juni 2023 kutoka asilimia 57 mwezi Juni 2022 jambo ambalo limechangia kurahisisha utoaji huduma nchini.

    Ameyasema hayo Septemba 27, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi na wahariri wa vyombo vya habari nchini chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.

  • MSD Yakabidhi Vifaa Tiba vya Mil. 500 - Hospitali ya Wilaya Kisemvule

    SERIKALI  kupitia Bohari ya Dawa (MSD), imekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 500 kwa hospitali ya Wilaya ya Ilala (Kivule), lengo ni kuboresha hali ya utoaji huduma wilayani humo.

    Vifaa hivyo ni pamoja na Vitanda vya kulalia wagonjwa, ventileta za ICU, viti mwendo, friji za kuhifadhia damu na sampuli, vitanda vya uchunguzi, Sunction machine, Ultra Sound machine, magodoro na mashuka.

  • Dkt. Mollel Apongeza Maboresho ya Huduma za MSD

    MTWARA.

    NAIBU Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amesema ameridhishwa na mabadiliko yanayofanywa na Bohari ya Dawa (MSD) hususani katika utendaji na utekelezaji wa mikataba ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba nchini.

    Dk. Mollel amesema hayo jana mkoani Mtwara katika ziara ya kikazi akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. John Jingu walipotembelea ofisi za Bohari ya Dawa Kanda ya Mtwara, kujionea hali ya utoaji wa huduma na changamoto ya ufinyu wa ghala unaoikabili kanda hiyo.

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.