Skip to main content

Wadau na wateja wa MSD wamekumbushwa kuendelea kushirikiana

Wadau na wateja wa MSD wamekumbushwa kuendelea kushirikiana kwa karibu ili kihakikisha wanaendelea kuboresha upatikanaji wa bidhaa  za afya nchini na kuwa utaratibu wa kulipa madeni ili kuiwezesha MSD kuwa na mtaji mzuri wa kuendelea kununua bidhaa za afya.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt.Charles Rashid Mkombachepa alipokuwa anafungua kikao cha mwaka cha wadau na wateja wa MSD kanda ya Kilimanjaro wa mkoani wa Arusha. Dkt. Mkombachepa amewakumbusha watendaji hao kuwa ubora wa huduma za MSD tunazoziona leo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya umechangiwa na upatikanaji mzuri wa fedha za kuiendesha MSD.

Hata hivyo Dkt. Mkombachepa ameipongeza MSD kwa kuboresha huduma kwa mkoa wa Arusha ambapo huduma hizo zilizoboreshwa zimewezesha kuongezeka kwa upatikanaji wa bidhaa za afya hadi kufikia zaidi ya asilimia 90%.

Dkt.Mkombachepa amesema kutokana na maboresho hayo ambayo MSD inayafanya, malalamiko yamepungua, lakini amesisitiza kuwa ni vizuri tukakaa pamoja na kutatua changamoto chache zilizobakia ili  kuzungumzia maboresho zaidi kuliko malalamiko.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fedha wa MSD Undule  Koroso amesema vikao hivi vina umuhimu kwa MSD kwani vinaboresha mahusiano na mawasiliano kati ya MSD na wataja wake na wateja wanapata wasaa wa kukutana ana kwa ana na MSD kuzungumza masuala ya kuboresha katika mnyororo mzima wa bidhaa za afya.

Add new comment

Restricted HTML

  • You can align images (data-align="center"), but also videos, blockquotes, and so on.
  • You can caption images (data-caption="Text"), but also videos, blockquotes, and so on.

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.