Skip to main content
     
13: 00 - 15:00
MSD HQ, Keko Mwanga

MSD Yapongezwa Ujenzi Viwanda vya Dawa na Vifaa Tiba

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Daniel Sillo, meipongeza Bohari ya Dawa (MSD) kwa jitihada kubwa inazozizifanya kuboreshaji upatikanaji wa bidhaa za afya nchini kwa kuanzisha viwanda vya kuzalisha dawa na kuboresha viwanda vya dawa vilivyokuwa na hali mbaya.

Sillo ametoa pongezi hizo leo, Kamati hiyo ilipokuwa ziarani MSD, ambapo pamoja na mambo mengine wajumbe wa Kamati hiyo walitembelea kiwanda cha dawa cha Keko, kiwanda cha MSD cha kuzalisha Barakoa pamoja na Maghala ya kuhifadhia bidhaa za afya dawa yaliyopo keko.

Amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa MSD Meja Jenerali Gabriel Mhidze na watendaji wote wa MSD kwa maono yao ya kuanzisha viwanda vya kuzalisha dawa na vifaa tiba kwani ununuzi bidhaa hizo kutoka nje ya nchi na kwingineko umekuwa ukiigharimu serikali fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kuboresha huduma nyingine.

Kamati yetu imesikia changamoto kutoka kwenu zinazowakwamisha kusonga mbele, tunazichukua na kuzifikisha serikalini ili kuhakikisha MSD inaimarika ipasavyo ili kuwezesha upatikanaji wa dawa nchini.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD Meja Jenerali Gabriel Mhidze katika taarifa yake ya utendaji aliyoiwasilisha kwa Kamati hiyo ameeleza kuwa pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikabili MSD bado inaendelea kutoa huduma bora na za kiwango cha juu kwa wananchi na kusimamia mnyororo wa ugavi, ili kuleta tija kwenye mfumo wa afya wa nchi.

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.