Skip to main content
     
13:00 - 16:00
MSD HQ, Keko Mwanga

Mkurugenzi Mkuu MSD, Awafunda Wataalamu Sekta ya Afya

Mkurugenzi Mkuu wa MSD Meja Jenerali Gabriel Saul Mhidze amesema kuwa na wataalam wa ndani wanaomudu kutumia vifaa vya maabara na kuvikarabati wenyewe ni hatua nzuri itakayopunguza gharama. 

Ameyasema hayo alipozungumza na Wataalamu wa maabara, Mafundi Sanifu na Wahandisi vifaa tiba kutoka MSD,Halmashauri na Hospitali mbalimbali nchini, ambao wapo kwenye mafunzo ya namna ya kufunga, kutumia na kuzifanyia matengenezo mashine mbalimbali za maabara ambazo zinatarajiwa kufungwa nchi nzima. Mashine hizo za maabara zitapunguza gharama za vipimo vya uchunguzi wa magonjwa kwa zaidi ya asilimia hamsini.

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.