Skip to main content
Global CEO - Fund, Visits MSD

Mtendaji Mkuu Global - Fund, Atembelea MSD

Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Dunia (Global fund) Bw. Peter Sands, amefanya ziara Bohari ya Dawa (MSD) na kujionea namna MSD inavyotekeleza majukumu yake.

Kupitia ziara hiyo, Mtendaji Mkuu huyo, amepata wasaa wa kutembelea maghala ya kuhifadhia bidhaa za afya, yanayomilikiwa na MSD, yaliyoko Keko, jijini Dar es Salaam.

Bwana Sands ameahidi kuwa mfuko huo utaendelea  kuiwezesha MSD kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya, hasa za miradi Msonge, huku akiipongeza MSD kwa kufanikisha usambazaji wa vyandarua nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bw. Mavere Tukai amemshukuru Bw. Sands kwa kuendelea kushirikiana na MSD katika nyanja mbalimbali za mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya, huku akibainisha maboresho mbalimbali yanayofanywa MSD kwasasa kuwa ni pamoja na kuimarisha uhifadhi kwa kuongeza maghala, kuimarisha mifumo ya uhifadhi, tehama na kuongeza baadhi ya watumishi katika kada mbalimbali kulingana na mahitaji ya majukumu ya MSD.

Ameongeza kuwa, maeneo mengine ni pamoja  na kuimarisha manunuzi ya bidhaa za afya, ufuatiliaji pamoja na uwezo wa kuchambua na kuchakata taarifa, sambamba na ukuzaji wa mtaji wa MSD.

Katika hatua nyingine, Mavere amebainisha kwamba MSD imeendelea kufanikiwa katika ununuzi na usambazaji wa bidhaa za miradi misonge, sambamba na kufanyia kazi hoja mbalimbali zilizo ibuliwa na Mkaguzi Mkuu wa mfuko huo.

Add new comment

Restricted HTML

  • You can align images (data-align="center"), but also videos, blockquotes, and so on.
  • You can caption images (data-caption="Text"), but also videos, blockquotes, and so on.

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.