Skip to main content

MSD YATUNUKIWA TUZO YA UMAHIRI WA UTOAJI HUDUMA

Bohari ya Dawa (MSD), imetunukiwa tuzo ya umahiri wa utoaji huduma kwenye sekta ya Famasi nchini (Award of Service Excellence in Pharmaceutical Sector) kupitia tuzo za mwaka za Tanzania Service Excellence Award 2024, zilizoandaliwa na taasisi ya Charted Institute of Customer Service (CICM) Tunzo hizo zimetolewa hapo jana na taasisi hiyo katika hafla maalum iliyofanyika katika ukumbi wa Holiday In, jijini Dar es Salaam 

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Kaimu Meneja wa Huduma kwa Wateja wa MSD Gendi Machumani amesema kupata tuzo ya utoaji huduma bora katika sekta ya afya inaonyesha jinsi jamii inavyothamini huduma bora zinazotolewa na MSD. Hatua hii inadhihirisha  mabadiliko makubwa ya kitaasisi chini ya Mkurugenzi Mkuu Mavere Tukai, ambapo taasisi imeweza kufanya kazi kwa ufanisi na kutimiza malengo ya kuhakikisha tunaboresha mnyonyoro wa ugavi wa bidhaa za afya nchini.

Ameongeza kuwa tuzo hii  inawafanya kuendelea kuwajibika kwa ufanisi na kuhakikisha afya za Watanzania zinalindwa  kwa kupeleka bidhaa za afya zenye ubora na gharama nafuu na kwa wakati.

Add new comment

Restricted HTML

  • You can align images (data-align="center"), but also videos, blockquotes, and so on.
  • You can caption images (data-caption="Text"), but also videos, blockquotes, and so on.

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.