Skip to main content

MSD Yashiriki Shughuli za Kijamii na Kutembelea Wateja Wake, Ikiadhimisha Miaka 30 ya Utendaji Toka Ianzishwe

Katika maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja kwa mwaka huu 2024, ambayo yalienda sambamba na sambamba na shughuli za kuadhimisha miaka 30 ya MSD, jumla ya wateja 18 walitembelewa kupitia kanda zote za MSD na kujadiliana masuala mbalimbali ya kuboresha Huduma zinazotolewa na MSD pamoja na mahusiano na ushirikiano na wateja.

Akizungumza baada ya shughuli hizo Mkurugenzi wa Ugavi na Uendeshaji Victor Sungusia ameeleza kuwa, kwa kuwa MSD inathamini mchango mkubwa wa mawazo yanayotolewa na wateja wake katika kufanya maboresho ya utoaji huduma, waliamua kuwafuata vituoni, badala ya kusubiri mikutano ya wadau ili pia kujionea hali halisi ya huduma wanazotoa, hasa kupata mrejesho wa vifaa walivyosambaza.

Katika maeneo yote ya wateja yaliyotembelewa na MSD, wadau na wateja wa MSD wameeleza kuridhishwa kwao na juhudi za uongozi wa MSD kufanya maboresho ya huduma na kiutendaji kwa ujumla, wakirejea hali halisi ya kuridhika kwa upatikanaji wa bidhaa za afya vituoni, ambao hadi sasa kwa wastani umefikia asilimia 92.

Aidha wateja hao wameeleza kuridhishwa na mifumo ya mawasiliano baina yao na MSD, ubora wa bidhaa za afya zinazonunuliwa na kusambazwa na MSD, bidhaa za afya kufika kwa wakati, kuimarisha mifumo ya mnyororo wa ugavi tangu kuomba bidhaa za afya hadi kupokea na kuleta vifaa na mashine za kisasa ambazo awali ilikuwa tabu kuzipata.

Mbali na kutembelea wateja, baadhi ya wateja wa MSD walitembelea Kanda zetu na kujionea namna MSD inavyotekeleza majukumu yake ya mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya, ambapo pia walitembelea maghala ya kuhifadhia bidhaa za afya na kuona shughuli nzima za kupokea na kuhifadhi na kutoa bidhaa za afya zinavyofanywa ghalani.

Mara baada ya ziara zote mbili, MSD pamoja na wadau na wateja wao kwa pamoja walikata keki na kula pamoja, kama ishara ya kuimarisha ushirikiano baina ya pande hizo mbili. Baadhi ya Kanda pia zilikabidhi bidhaa za afya zilizokuwapo kwenye kalenda ya mgawo, kukabidhi zawadi mbalimbali, misaada na kupata chakula cha pamoja na wadau.

Katika hatua nyigine Kanda zote za MSD, zilishiriki matendo ya huruma kwa kutoa misaada mbalimbali ya kijamii kwa wahitaji (CSR) katika hospitali

Add new comment

Restricted HTML

  • You can align images (data-align="center"), but also videos, blockquotes, and so on.
  • You can caption images (data-caption="Text"), but also videos, blockquotes, and so on.

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.