Skip to main content
Officials from MSD, (first left, and second right), handing over Medical Equipment Documents to the Chief Medical Officer of Dar es Salaam City

MSD Yakabidhi Vifaa Tiba vya Mil. 500 - Hospitali ya Wilaya Kisemvule

SERIKALI  kupitia Bohari ya Dawa (MSD), imekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 500 kwa hospitali ya Wilaya ya Ilala (Kivule), lengo ni kuboresha hali ya utoaji huduma wilayani humo.

Vifaa hivyo ni pamoja na Vitanda vya kulalia wagonjwa, ventileta za ICU, viti mwendo, friji za kuhifadhia damu na sampuli, vitanda vya uchunguzi, Sunction machine, Ultra Sound machine, magodoro na mashuka.

Akizungumza wakati wa kupokea vifaa hivyo, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Dk. Zaituni Hamza, ameishukuru serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa ujio wa vifaa hivyo, kwani vinaakisi adhma na dhamira ya kuboresha huduma za afya nchini.

Aliongeza kuwa, huduma za mama na mtoto kwasasa zimeboreka kuliko wakati mwingine wowote, hali ambayo inasababisha kupungua kwa vifo vya wajawazito na watoto wachang wakati wa kujifungua.

Katika hatua nyingine, alimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai, kwa maboresho ya huduma, ambapo kwa sasa zimeimarika, mawasiliano yameboreshwa kati ya bohari na wateja wake hali inayosababisha hospitali kupata msaada wa haraka pale wanapokua na uhitaji.

Add new comment

Restricted HTML

  • You can align images (data-align="center"), but also videos, blockquotes, and so on.
  • You can caption images (data-caption="Text"), but also videos, blockquotes, and so on.

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.