Mkurugenzi Mkuu MSD, Afanya Mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA (CEO)
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw.Mavere Ali Tukai amefanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Bw.Eliakim C.Maswi kuhusu namna bora ya kuboresha ununuzi wa bidhaa za afya kufuatia changamoto kadhaa zinazoikabili Bohari ya Dawa katika eneo hilo.
Mavere amemueleza Mtendaji Mkuu huyo mtazamo wake kuhusu manunuzi katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria, taratibu, miongozo na mfumo wa TANEPS.
Kupitia mkutano huo, Mavere amebainisha changamoto mbalimbali zinazoikabili Bohari ya Dawa katika masuala ya manunuzi, na namna bora ya kuzitatua, ili kuboresha upatikanaji wa Dawa na Vifaa Tiba nchini.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA amempongeza Bw.Mavere kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo huku akiahidi kuzifanyia kazi haraka changamoto mbalimbali za manunuzi zinazoikabili MSD.
Ununuzi wa Umma
Aidha, alisisitiza kuwa taasisi za umma zina mahitaji tofauti, hivyo kuahidi kuangazia na kutatua changamoto zilizoainishwa ili kuboresha manunuzi ya umma.