Skip to main content

Mganga Mkuu Mkoa wa Pwani, Apongeza Ushirikiano Baina ya MSD na Wateja Wake.

Bohari ya Dawa(MSD) Kanda ya Dar es Salaam imeandaa kikao kazi na wadau wake wa mkoa wa Pwani kilichofanyika Mkoani Pwani - Wilayani Kabaha katika Chuo cha Mwalimu Nyerere  kuzungumza kwa pamoja namna ya koboresha upatikanaji wa bidhaa za afya.

Akizungumza kwenye kikao hicho Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Dkt. Urio Kusirye amesema vikao kazi hivyo ni muhimu kwani vinachangia kuhakikisha huduma za afya ndani ya Mkoa wa Pwani zinakuwa endelevu na bora.

 “Tunapaswa kuwa na vikao kama hivi ili kuhakikisha changamoto zote ambazo zinajitokeza katika utendaji wetu wa kila siku zinazungumzwa kwa pamoja na kutatuliwa kwa pamoja”.

Hata hivyo, Dkt. Kusirye  ameongeza kuwa ukilinganisha walipotoka na walipo sasa, MSD kwa kiasi kikubwa imeboresha huduma zake akieleza kuwa bidhaa za afya ambazo hapo awali zilikuwa zinapatikana kwa kiasi kidogo sasa zinapatikana vizuri  kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. 
“Tunakubali kuwa tunachangamoto kadhaa za kiutendaji ambazo zinaweza kutatuliwa kwa kukutana sisi kwa pamoja na kuwekeana mikakati ya namna ya kutatua changamoto hizo." Aliongeza Dkt. Kusirye

Naye Meneja Kanda ya Dar es Salaam Bi. Betia Kaema amesema kwenye kikao hicho wamewekeana  maazimio na wadau wao ambao wanawahudumia wa Mkoa wa Pwani, ambapo maazimio hayo yatakuja kupimwa mwaka wa fedha ujao ili kujua yale yaliyofanyiwa kazi.

Aidha ameongeza kuwa MSD inapoadhiadhimisha miaka 30 ya huduma toka ianzishwe, imekuwa ikifanya maboresho kadha wa kadha ili kuhakikisha malengo ya kumuhudumia mtanzania wa kawaida yanafikiwa kwani, kama kauli mbiu ya MSD isemavyo, "Tmedhamiria Kuokoa Maisha".

Ameongeza kuwa wao kama kanda ya Dar es salaam, wamejipanga kuhakikisha wanatoa huduma bora na kwa weledi, kwa kuhakikisha bidhaa za afya zinapatikana kwa wakati na kuwafikia walengwa, kwani hiyo ndio Tanzania inayotakiwa kutokana na maboresho makubwa yaliyofanyika nchini katika sekta ya afya, ikiwemo maboresho ya miundombinu ambayo ni sharti yaende sambamba na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.

Add new comment

Restricted HTML

  • You can align images (data-align="center"), but also videos, blockquotes, and so on.
  • You can caption images (data-caption="Text"), but also videos, blockquotes, and so on.

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.