Skip to main content
Manyara Regional Chief Medical Officer Dr. Andrew Method Speaking to Health Sector Executives, During a Stakeholder Meeting Between MSD and Its Stakeholders

RMO Manyara - Avitaka Vituo vya Kutolea Huduma za Afya Kulipa Madeni ya MSD

Watendaji kwenye vituo vya kutolea huduma za afya waliopo kwenye Mkoa wa Manyara wamekumbushwa kuendelea na utaratibu wa kulipa madeni ya Bohari ya dawa (MSD) kwani kufanya hivyo ni kuiwezesha MSD kuwa na mtaji mzuri wa kuendelea kununua bidhaa za afya ambazo zinasambazwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini. 

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt. Andrew Method alipokuwa  anafungua kikao cha wadau na wateja wa MSD kanda ya Kilimanjaro wa mkoani wa Manyara.  

Dkt. Method amewakumbusha watendaji hao kuwa ubora wa huduma za MSD tunazoziona leo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya umechangiwa na upatikanaji mzuri wa fedha za kuiendesha MSD.

Pamoja na kulipa madeni yetu kwa MSD, lakini tuendelee kufanyakazi kwa ukaribu na taasisi yetu hii na pale penye changamoto basi ni vizuri tukakaa nao kutatua ili kuondoa malalamiko kwa wapokea huduma ambao ni wananchi alisema Dkt. Method.

Hata hivyo Dkt. Method ameipongeza MSD kwa kuboresha huduma kwa Mkoa wa Manyara ambapo huduma hizo zilizoboreshwa zimewezesha kuongezeka kwa upatikanaji wa bidhaa za afya hadi kufikia asilimia 95% .  

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Dkt. Vicent Gyunda  ambaye ni mshiriki wa kikoa hicho cha wadau amesema vikao hivi vinaisaidia MSD kwanza kupata mrejesho kutoka kwetu ambao ni wateja wao lakini vilevile vikao hivi vinasaidia kuongezeka kwa bidhaa za afya kwa asilimia 98% katika Wilaya ya Kiteto.

Add new comment

Restricted HTML

  • You can align images (data-align="center"), but also videos, blockquotes, and so on.
  • You can caption images (data-caption="Text"), but also videos, blockquotes, and so on.

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.