Skip to main content
Minister of Health Hon. Ummy Mwalimu Opening a Meeting Between MSD and Its Stakeholders, Who Are Manufacturers, Distributors and Marketers of More Than 200 Health Products From Within and Outside the Country.

MSD Yateta na Wazalishaji, Wasambazaji na Washitiri wa Bidhaa za Afya.

Bohari ya Dawa (MSD) imekutana na wazalishaji, wasambazaji na washitiri wa bidhaa za afya zaidi ya 200 kutoka nje na ndani ya nchi kujadiliana namna ya kuboresha ushirikiano na kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya nchini.

Katika hafla hiyo Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amewaeleza wadau hao kuwa serikali inaendelea kuboresha ushirikiano na sekta binafsi kuchagiza uanzishaji wa viwanda vya bidhaa za afya nchini.

Nia kubwa ni kupunguza matumizi ya fedha za kigeni kununua bidhaa za afya kutoka nje ya nchi, ambapo kwa sasa asilimia 85 ya bidhaa hizo zinatoka nje ya nchi.

Kwa upande wake Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu ameeleza kuwa ofisi yake ipo tayari kuiunga mkono MSD katika uanzishwaji wa viwanda vya bidhaa za afya  kwa kushirikiana na sekta binafsi, kwani ni miongoni mwa  maeneo yanayopewa kipaumbele na serikali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Rosemary Silaa amesema kukaa na wadau na kujadiliana ni jambo muhimu katika kuboresha huduma, huku Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai akieleza kuwa mifumo ya ununuzi imeboreshwa ikiwa ni pamoja na kuingia mikataba ya muda mrefu na wazalishaji.

Add new comment

Restricted HTML

  • You can align images (data-align="center"), but also videos, blockquotes, and so on.
  • You can caption images (data-caption="Text"), but also videos, blockquotes, and so on.

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.