Skip to main content
MSD Receives a Shipment of HIV and Syphilis Tests

MSD Yapokea Shehena ya Vipimo vya UKIMWI na Kaswende

Katika kuadhimisha Siku ya UKIMWI Duniani MSD imeendelea kupokea na kusambaza bidhaa mbalimbali za afya za kupambana na kudhibiti maambukizi ya Virusi vya UKIMWI Pamoja na Kaswende.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai ameeleza kuwa miongoni mwa bidhaa za afya ambazo kwa sasa inauhitaji mkubwa na inaendelea kusambazwa na MSD kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ni vipimo vya kupima maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na gonjwa la zinaa la Kaswende (HIV/ Syphilis Duo).

Vipimo hivyo vinafadhiliwa na Mfuko wa Dunia wa kupambana UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria (The Global Fund) na pia hutumika kupima akina mama wajawazito kutambua maambukizi ya magonjwa yote mawili kwa wakati mmoja.

Kwa mujibu wa Dr. Ibadi Kaondo wa MSD, vipimo hivyo vinamsaidia mama mjamzito kutambua hali ya afya mapema, na endapo maambukizi yamegundulika inarahisisha kuanza matibabu mapema ili kufubaza makali ya virusi vya ukimwi na kutibu kaswende kwa ajili kuimarisha afya ya mzazi na kumkinga mtoto dhidi ya Maambukizi ya VVU, Kaswende ama kujifungua mtoto mfu.

Hapo awali vipimo hivi kila kimoja kilikuwa kinajitegemea, ambapo vilitumia muda mrefu kutoa majibu. MSD kwa sasa ina shehena ya kutosha ya vipimo hivyo ambavyo tayari baadhi vilishaanza kusambazwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Maadhimisho ya kitaifa ya siku ya UKIMWI duniani kwa mwaka 2022, yamefanyika katika viwanja vya Ilulu Mkoani Lindi, yakihudhuriwa na viongozi na wadau mbalimbali huku mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Add new comment

Restricted HTML

  • You can align images (data-align="center"), but also videos, blockquotes, and so on.
  • You can caption images (data-caption="Text"), but also videos, blockquotes, and so on.

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.