Skip to main content

MSD Yakabidhi Vifaa vya Upasuaji Vyenye Thamani ya Milioni 210 - Itigi

Bohari ya Dawa (MSD) kupitia Kanda ya Dodoma  leo imekabidhi vifaa vya  upasuaji kwa hospitali ya Wilaya ya Itigi, iliyoko mkoani Singida, vyenye thamani ya jumla ya shilingi milioni 210.

Akipokea vifaa hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Dkt.Vicent Mashinji amesema nia ya serikali kununua vifaa hivyo ni kuhakikisha huduma za afya zinatolewa kwa viwango vinavyokubalika, na kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika hasa kwa mama na watoto wakati wa kujifungua.

Mkuu huyo wa Wilaya ameeleza kuwa baada ya majengo ya hospitali kukamilika,wakaamua kununua vifaa hitajika ili waanze kuhudumia wananchi, kwani kabla ya ujio wa Vifaa hivyo iliwalazimu wananchi kusafiri umbali mrefu kwaajili ya kupata huduma za upasuaji.

Halikadhalika Mhe. Mashinji amebainisha kuwa kwa ujio wa Vifaa tiba hivyo, serikali imewaondolea mzigo wa gharama kubwa wananchi wa Itigi, kwani awali walikuwa wakitumia gharama kubwa kupata huduma za upasuaji kutoka hospitali binafsi hivyo ni dhahiri huduma hizo zinaenda kutolewa kwa gharama nafuu hospitalini hapo.

Katika hatua nyingine Dkt. Mashinji amewataka wataalamu wanaotumia vifaa hivyo kuhakikisha wanavitunza na kuvitumia vizuri ili vidumu, kwani ni dhahiri serikali imetoa pesa nyingi kuvigharamia.

Kwa upande wake Meneja wa kanda ya MSD Dodoma Mwanashehe Jumaa, ameeleza kuwa walipokea shilingi milioni 300 kwa ajili ya vifaa vya hospitali hiyo, na wamekabidhi leo vifaa vya shilingi mill. 210 na vifaa vilivyosalia vitakabidhiwa hivi karibuni.

Bi. Jumaa amebainisha kwamba miongoni mwa vifaa hivyo ni pamoja na mashine ya usingizi, mashine za oxygen ,mashine ya kufulia, jokofu la kuhifadhia dawa, taa za chumba cha upasuaji, vitanda vya upasuaji na vifaa vya kuhifadhia watoto njiti.

Nao wananchi wa Wilaya ya Itigi, kwanyakati tofauti wameishukuru serikali kwa kuwajengea hospitali ya Wilaya na kuwaletea Vifaa tiba, kwani imewatua mzigo mzito wa huduma ghari za afya, uliokuwa umewaelemea.

Add new comment

Restricted HTML

  • You can align images (data-align="center"), but also videos, blockquotes, and so on.
  • You can caption images (data-caption="Text"), but also videos, blockquotes, and so on.

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.