Skip to main content

Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD, Aipongeza Kanda ya MSD Tanga kwa Kuvuka Malengo ya Mauzo

Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) Dkt. Rukia Mwifunyi amepongeza Kanda ya MSD Tanga kwa kuvuka malengo ya mauzo, katika robo mwaka ya kwanza ya mwaka kwa asilimia 12.

Mjumbe huyo wa Bodi, ambaye ni mlezi wa Kanda ya MSD TANGA amefuatana na  Meneja Huduma za Sheria MSD, Elisamehe Macha katika ziara ya kutembelea wateja wanaohudumiwa na Kanda ya Tanga,ziara ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka thelathini (30) ya utendaji wa MSD tangu kuundwa kwake.

Akizungumza na watumishi wa kanda ya Tanga Dkt. Mwifunyi amemwelekeza Meneja wa kanda ya Tanga, Sitti Abdurahman kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu madeni wanayowadai wateja wao.

Naye Meneja wa Kanda hiyo Bi. Sitti Abdulahman amesema Kanda hiyo imejipanga kimkakati kuhakikisha inakidhi matakwa ya wateja wake, kwa kuhakikisha inakuwa na bidhaa za afya wakati wote na kuwahudumia wateja kwa weledi mkubwa.

Aidha, ameongeza kuwa Kanda hiyo pia imejidhatiti katika kuhakikisha inafuatilia madeni yake, na kuhakikisha inapunguza madeni ya wateja wake, ili kuipa MSD msuli wa kuendelea kuagiza bidhaa za afya.

Ziara hiyo inaendelea kwa kutembelea Hospitali ya mkoa Bombo, na kituo cha afya Nkumba  kilichopo wilaya ya Muheza, Tanga, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho maalum ya miaka 30 ya MSD, toka ilipoanzishwa mnamo mwaka 1994.

Add new comment

Restricted HTML

  • You can align images (data-align="center"), but also videos, blockquotes, and so on.
  • You can caption images (data-caption="Text"), but also videos, blockquotes, and so on.

About

MSD ilianzishwa kwa madhumuni ya uzalishaji, ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya zilizoidhinishwa zinazohitajika kutumiwa na vituo vya afya. Katika kutekeleza dhamira hii, tunahakikisha kuwa bidhaa za afya nchini Tanzania zinapatikana, zinategemewa, na zinauzwa kwa bei nafuu lakini pia zinatolewa kwa wakati katika vituo vyote vya afya nchini Tanzania na kwingineko.

Featured Posts

Contact info

Dhamira yetu: Kufanya bidhaa bora za afya kufikiwa na vituo vyote vya afya vya umma nchini Tanzania.