MSD na Wadau wa Afya Mkoa wa Dar es Salaam Wahimizwa Kushirikiana
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Bi.Rehema Madenge, amewataka wadau wa afya mkoani humo, kushirikiana kwa karibu na Bohari ya Dawa (MSD) ili kuboresha huduma na kutatua changamoto mbalimbali zinazoukabili mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya mkoani humo.