Uzalishaji wa Bidhaa za Afya
Katika kuongeza ufanisi wa usimamizi wa shughuli za uzalishaji na kuhakikisha utekelezaji wa miradi kwa wakati, MSD imeanzisha Kampuni Tanzu inayoitwa “MSD Medipharm Manufacturing Company Limited” ambayo inajukumu la kusimamia shughuli za uzalishaji wa bidhaa za afya na itakuwa na uwezo wa kuingia ubia na wawekezaji wengine. Kwa sasa kampuni hii inasimamia viwanda vya Barakoa (Surgical na N95 Mask) Dar es salaam na kiwanda cha Mipira ya Mikono Idofi Makambako, Mkoani Njombe.