MSD Yapongezwa kwa Maboresho ya Huduma Zake Mkoani Kagera
Bohari ya Dawa (MSD) imepongezwa kwa kuimarisha mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya mkoani Kagera, ambao umepunguza malalamiko ya upungufu wa bidhaa za afya mkoani humo.
Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa huo Steven Nashauri Ndaki, wakati akizungumza na ujumbe maalum kutoka MSD uliomtembelea ofisini kwake, ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Bi. Rosemary Silaa, ikiwa ni ziara maalum ya kuadhimisha miaka 30 ya MSD.