Ujumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Watembelea Hospitali za Mkoa wa Simiyu
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Bw. Ally Seleman, akiambatana na Kaimu Meneja Mipango,Tathimini na Ufuatiliaji leo tarehe 20/11/24 wametembelea Kanda ya MSD Mwanza na kujionea jinsi Kanda hiyo inavyotekeleza majukumu yake, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa MSD.
Kupitia ziara hiyo Bw. Selemani amepokea taarifa ya utendaji wa Kanda hiyo, sambamba na mipango mbalimbali ambayo Kanda hiyo imejiwekea Ili kuhakikisha inaboresha huduma zake.