Dkt. Philip Mpango Aweka Jiwe la Msingi Kiwanda cha Mipira ya Mikono cha MSD, Kilichopo Idofi Makambako Mkoani Njombe
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amesema serikali inatambua vita iliyopo katika ujenzi wa viwanda vya dawa lakini kwa kuwa uwamuzi huo ni wa Rais Dk. Samia Suluhi Hassan hakuna atakayefanikiwa kuvikwamisha hivyo vitajengwa.
Amesema kwa sasa serikali inaagiza dawa kwa asilmia 80 na vifaa tiba kwa asilimia 90 kutoka nje ya nchi, hali inayosababisha uhaba wa vifaa na gharama kubwa za uagizaji wa vifaa vya afya hivyo ni lazima kuchukua maamuzi magumu.