Skip to main content
 • Viongozi wa Sekta ya Afya Wahimizwa Kushirikiana na MSD

  MOROGORO.

  Wasimamizi na wadau wa afya mkoani Morogoro, wameaswa kushirikiana kwa ukaribu na Bohari ya Dawa (MSD), ili kwa pamoja waweze kutatua na kuboresha hali ya upatikanaji wa bidhaa za afya mkoani humo, kwa ajili ya ustawi watu na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

  Rai hiyo imetolewa hii leo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wà Morogoro, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mjini Mhe. Rebeka Nsemwa, wakati akifungua kikao kazi cha wateja na wadau wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, kilichokutanisha viongozi wa sekta ya afya ngazi ya mkoa na wilaya mkoani humo.

 • SADC Yazindua Kanzidata ya Mfumo wa Taarifa za Bidhaa za Afya Kwa Nchi Wanachama.

  Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) imezindua Kanzidata maalumu kwaajili ya ukusanyaji na uchakataji wa taarifa za Dawa na vifaa tiba kutoka kwa wazalishaji na wazabuni mbalimbali Duniani, ambapo mfumo huo utarahisisha upatikanaji na ununuzi wa bidhaa za afya kutoka kwa nchi wanachama.

 • Wataalamu wa Afya Kutoka Sierra Leone, Wafanya Ziara ya Mafunzo MSD

  Wataalamu wa Afya kutoka nchini Sierra Leone leo wametembelea Bohari ya Dawa (MSD) kwa lengo kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu shughuli za Ugavi, Uhifadhi, Uendeshaji, Ununuzi, Huduma kwa Wateja, Sera, Udhibiti Ubora, pamoja na mambo mengine yanayohusu mnyororo wa Ugavi wa bidhaa za afya.

  Akiongea kwa niaba ya Wizara ya Afya wakati wa kuukaribisha ujumbe huo nchini, Mfamasia Mkuu wa Serikali Daudi Msasi, amesema ujio wa wageni hao ni ishara kwamba kama nchi tumeboresha na kuimarisha Bohari yetu katika utoaji wa huduma, ndio maana wengine wanakuja kujifunza.

 • Somalia Kushirikiana na MSD, Ununuzi wa Bidhaa za Afya

  Rais wa Somalia Mheshimiwa Hassan Sheikh Mohamud amesema nchi yake imeamua kushirikiana kwa karibu na Bohari ya Dawa ya Tanzania katika ununuzi wa bidhaa za afya na kubadilishana uzoefu wa namna mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya unavyofanya kazi.

  Rais Mahamud ambaye yuko ziarani nchini Tanzania, ameyasema hayo alipoitembelea MSD, na kuongeza kuwa kutokana na uzoefu wa MSD, wana uhakika kuwa ubora wa bidhaa za afya utakuwa wa uhakika.

 • Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Aipongeza MSD kwa Maboresho ya Huduma

  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameupongeza uongozi wa Bohari ya Dawa (MSD) kwa mabadiliko makubwa yanayoendelea katika taasisi hiyo, ambayo kwa kiasi kikubwa yamewezesha kupunguza malalamiko ya uhaba wa bidhaa za afya nchini, mathalani malalamiko ya uhaba wa dawa.

  Mhe. Senyamule ameeleza kwamba awali wakienda kwenye mikutano ya hadhara kuongea na wananchi, walikumbana na malalamiko mengi ya uhaba wa dawa, lakini hivi karibuni hali imebadilika, japokuwa bado kuna changamoto, lakini angalau inatia moyo kuona kuna mageuzi yanafanyika.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.