Usimamizi wa Vihatarishi
Usimamizi wa Vihatarishi unalenga kupunguza madhara na kuongeza fursa zitakazoisaidia MSD kuweza kufikia malengo yake ya kimkakati. Mfumo wa Usimamizi wa vihatarishi umewekwa kwa uwazi ukitarajia uwepo wa vihatarishi, tathmini yake na na namna ya kuweza kuviepuka vile vyenye madhara na kutumia fursa kwa vile vyenye kuleta tija na ufanisi. Usimamizi wa Vihatarishi MSD unazingatia njia zinazoweza kukinga na kuifanya Taasisi kuwa himilivu kutoka kwenye madhara mbalimbali yanayotokana na mifumo, watu na shughuli mbalimbali za Taasisi. Miongoni mwa njia zinazotumika ni mifumo ya Bima, utambuzi na mingineyo.
Bohari ya Dawa inatumia Miongozo mbalimbali ya usimamizi wa vihatarishi nchi na ile ya Kimataifa ili kusaidia Taasisi kufanya maamuzi yake kwa usahihi na kutumia rasilimali ipasavyo ikiwa na malengo ya kufikia matarajio ya wateja. Mfumo huu wa usimamizi wa vihatarishi unawezesha watumishi wa Bohari ya Dawa kufanya maamuzi kwa kuzingatia vihatarishi kwa kujiamini na kuzingatia uwezo wa Taasisi kuhimili vihatarishi hivyo.
Katika kufikia malengo ya Taasisi, MSD imegawa vihatarishi katika makundi matano ambayo ni; Vihatarishi vya Kimkakati, Fedha, Utendaji, Tehama na Kuzingatia Sheria, Taratibu Kanuni na Miongozo mbalimbali. Mgawanyo huu wa vihatarishi unalenga kuwezesha MSD kufikia matarajio ya wateja na wadau wengine, kwa kutimiza mahitaji yao kwa kutumia njia shirikishi, ukusanyaji wa rasilimali/ kupunguza gharama na matumizi ya TEHAMA.