Skip to main content

Somalia Kushirikiana na MSD, Ununuzi wa Bidhaa za Afya

Rais wa Somalia Mheshimiwa Hassan Sheikh Mohamud amesema nchi yake imeamua kushirikiana kwa karibu na Bohari ya Dawa ya Tanzania katika ununuzi wa bidhaa za afya na kubadilishana uzoefu wa namna mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya unavyofanya kazi.

Rais Mahamud ambaye yuko ziarani nchini Tanzania, ameyasema hayo alipoitembelea MSD, na kuongeza kuwa kutokana na uzoefu wa MSD, wana uhakika kuwa ubora wa bidhaa za afya utakuwa wa uhakika.

Naye Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu ameeleza kuwa kwa kuwa sasa Somalia ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania kupitia MSD itaweza kununua bidhaa za afya kwa pamoja ili kupata bidhaa hizo kwa bei nafuu.

Ameongeza kuwa, Marais wa nchi hizo mbili, yaani Tanzania na Somalia wamewapa maelekezo Mawaziri wa Afya nchi zao kukaa pamoja na kuangalia namna ya kushirikiana katika masuala ya upatikanaji wa bidhaa za afya kwa urahisi, kuzingatia ubora na kwa bei nafuu.

Kiongozi huyo wa Somalia na ujumbe wake alizungumza na viongozi wa Wizara ya Afya, Menejimenti ya MSD na kutembelea ghala la kuhifadhia dawa la makao makuu MSD.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.